Baada ya Sudan ya Kusini kujitenga kutoka main Sudan na kuongeza idadi za nchi katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla, inaonekana inaweza kuwa chachu kwa baadhi ya majimbo ama nchi kumegeka,
inaweza kuongeza nguvu kwa nchi zilizokuwa kwenye maelekeo huo na pia inawweza kuwa chachu kwa nchi/majimbo mapya, baadhi ya majimbo na nchi hizo ni kama ifuatavyo
1)TAnzania
Kwa hali ya kisiasa na nchi kukosa mwelekeo wa kujua ni kipi cha kushika kwanza, kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kutoka kwenye muungano,
2) DRC
Ni miongoni mwa Nchi kubwa kabisa Barani Afrika na duniani
Tatizo kubwa la DRC ni Majimbo yaliyogawanjwa kwa minajili ya ukabila, Congo DR pana ukabila mkali kabisa, Baadhi ya Province za Congo zimeendelea sana na sababu zinazotoka kwenye province ambazo ziko nyuma kimaendeleo ni kuwa hizo zimeendelea kutokana na viongozi
3) Morocco
Polisario wamepigana kwa miaka mingi mno kutaka kutoka Morocco na kuwa na nchi yao ya Sahara Magharibi, haya mapinduzi ya nchi za kiarabu na kupatikana kwa uhuru wa Sudan ya kusini ambao walikuwa almost wanafanana kwenye kutafuta uhuru wao,inawatia Chachu kubwa kwa watu wa sahara Magaharibi, kuongeza nguvu zao za kudai Nchi "yao"
4) Somalia na SomaliLand nchi inayojiendesha yenyewe lakini bado haijajitangazia uhuru wake,
5) Baada ile issue ya Biafra Nigeria inaonekana kana kwamba bado wapo Pamoja, lakini muendelezo wa siasa za Kidini na Kikabila zinaonyesha wazi uwezekano wa nchi kumegeka
mitizamo yenu ni ipi wana JF