Nchi nyingi zinazonunua ndege za kivita aina ya F-35 huuziwa toleo la kawaida, lenye udhibiti mkali. ni sawa na kununua simu ya mkopo au iliyofungiwa laini ya tigo au yas,
Israel ndiyo taifa pekee (isipokuwa Marekani yenyewe) linaloruhusiwa kufanya modifications za F-35 ikiwemo kuweka avionics system zao, Uncle Sam (Marekani) hufaidika kwa kupata maboresho hayo bila malipo.
Israel pekee ndiye aliyepewa F-35 toleo maalum, F-35I Adir, linaloruhusu:
- Kuweka software yao wenyewe
- Kuchagua na kuunganisha silaha zao
- Kutumia mbinu zao za kugundua na kupofusha rada
- Kutumia teknolojia yao kudanganya mifumo ya adui ionyeshe taarifa za uongo
- Toleo hili haliwezi kuzimwa wala kufuatiliwa na Marekani
Nchi nyingine hupata F-35 ya kawaida sana, yenye mipaka na utegemezi mkubwa kwa Marekani.
Katika migogoro ya hivi karibuni, ikiwemo mapigano ya siku 12 yanayohusishwa na Iran, F-35I Adir imeonyesha tofauti kubwa kabisa:
- Kuzima ulinzi wa anga: Adir ilifanikiwa kudhoofisha mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran, ikiwemo mifumo ya kisasa ya Urusi.
- Mashambulizi ya usahihi wa juu: Israel waliweza kushambulia malengo nyeti, wakiwemo viongozi wakuu wa kijeshi, kwa usahihi mkubwa kutoka umbali wa zaidi ya maili 100.
- Udhibiti wa anga: Marekebisho ya Israel, hasa katika vita vya kielektroniki, yaliwezesha kuzima na kuchanganya mifumo ya adui; ndege ziliruka juu ya anga la Tehran bila kuzuiwa huku mifumo ya Iran ikishindwa kufanya kazi ipasavyo.
- Usalama wa operesheni: Ndege zote zilirejea salama, hakuna hata moja iliyodhibitiwa au kupotea.
- Kujiamini kupitiliza hadi kutumia marubani wa kike: Marubani wa kike walikuwa wakikabidhiwa ndege Kwenda kupiga targets na kurudi salama
Kwa kifupi, si kila F-35 ni sawa, tofauti iko kwenye uhuru wa teknolojia na udhibiti wa matumizi. hata nchi zinazonunua zinaimezea sana mate F35 ya Israel, wanaona wanachopata ni robo ya ndege walizonazo Israel.
Unapoona Marekani inamng'ang'ania Israel ujue kuna jambo la ziada, wana share teknolojia kubwa sana