Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,103
Kutopewa uzito na nchi tajiri kikao cha Istanbul cha kuzisaidia nchi zenye ustawi mdogo
Kikao cha nne cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuzisaidia nchi zenye ustawi mdogo duniani kimefanyika mjini Istanbul Uturuki bila ya kupewa uzito unaostahiki na viongozi wa nchi tajiri na zilizoendelea. Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi tajiri na zilizoendelea hawakuonyesha hamu kubwa ya kuhudhuria kikao hicho wakati ambapo hakuna mwenye haki ya kujifanya kuwa hana jukumu wala dhima yoyote kuhusiana na mwanadamu ambaye hutumia dola 1.25 tu kwa siku ili kuweza kuendelea na maisha yake ya dhiki na hilaki. Waziri Mkuu wa Uturuki ameongeza kuwa leo masuala na matatizo ya dunia yamevuka mipaka, nchi, jiografia ya kisiasa na watu wa mataifa. Erdogan amesema matatizo ya hifadhi ya mazingira, hali mbaya ya ikolojia na hali ya hewa, ugaidi na uhajiri yanazitishia nchi zote, na kwamba nchi ambazo zinayapuuza matatizo hayo zinawafanyia dhulma wananchi wao wenyewe na jamii ya kimataifa pia. Waziri Mkuu wa Uturuki amesisitiza kuwa vita vya kupambana na njaa na umasikini si jukumu la mtu binafsi bali linaihusu jamii nzima ya kimataifa.
Kikao cha nchi zenye ustawi mdogo kimebuniwa na Umoja wa Mataifa; na hufanyika mara moja kila baada ya miaka kumi ili kufikiria njia mpya za kuzisaidia nchi masikini duniani. Imepangwa kuwa hati ya mkakati mpya wa kukabiliana na umasikini katika nchi zenye ustawi mdogo ipasishwe katika kikao cha Istanbul. Kikao cha nne cha nchi zenye ustawi mdogo kimefanyika katika hali ambayo takwimu zinaonyesha kuwa hali ya nchi hizo hivi sasa ni mbaya zaidi kulinganisha na miaka kumi iliyopita. Katika ripoti uliyotoa sambamba na kuanza kwa mkutano wa Istanbul, Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kuongezeka idadi ya nchi masikini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu katika nchi masikini zaidi duniani itafikia bilioni moja na milioni 700. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imefafanua kwamba kuongezeka kwa idadi ya watu katika nchi masikini kutaongeza matatizo zaidi katika utoaji huduma za msingi zikiwemo za afya na elimu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa asilimia 60 ya watu katika nchi hizo wana umri chini ya miaka 25, ambao kama watapatiwa fursa mwafaka, watu hao wa rika la vijana wanaweza kuwa injini ya kuongeza kasi ya ukuaji uchumi; vinginevyo watakabiliwa na ufukara wa kupindukia. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa nchi 48 ambazo zina idadi ya watu bilioni moja ziko kwenye orodha ya nchi masikini zaidi duniani. Thelathini na tatu kati ya hizo ziko katika bara la Afrika, 14 ni za bara la Asia na nchi ya 48 ni Haiti iliyoko katika bara la Amerika. Hii ni katika hali ambayo miaka 40 nyuma nchi 25 tu zilikuwa kwenye orodha ya mataifa masikini duniani. Idadi ya nchi masikini imeongezeka maradufu katika muda wa miongo minne iliyopita wakati ambapo kiwango cha uzalishaji wa utajiri na mazao ya kilimo kimeongezeka mara kadhaa. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kuna ufa mkubwa wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi tajiri za Kaskazini na zile masikini za Kusini. Na hii ni katika hali ambayo katika vikao mbalimbali vilivyofanyika katika miongo kadhaa iliyopita nchi tajiri na hasa zile za kikoloni zimekuwa zikitoa ahadi ya kuzisaidia nchi masikini na kupunguza idadi ya watu masikini. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa ahadi hizo zilikuwa ni za makaratasini tu, na kama kuna msaada ambao umetolewa, basi ni kwa malengo ya kujipatia faida na maslahi ya muda mrefu katika nchi masikini. Tunachoweza kusema ni kwamba kutokana na hatua ya nchi tajiri na zilizoendelea ya kutokipa uzito unaostahiki kikao cha Istanbul hatuwezi kuwa na matumaini makubwa kuwa malengo yaliyomo kwenye hati ya kikao hicho kuhusiana na kuboresha hali ya maisha katika nchi masikini yataweza kufikiwa.../