Umekuwa ni msiba mkubwa ambao ulilikumba Taifa hili lililobarikiwa utajiri wa kupigiwa mfano na unaotamaniwa na wapenda vinono duniani kote, Sasa yapata takriban miaka 58 imezikwa na hadi Leo inasadikika kuwa bado inapumua kwa shida shimoni(Kaburini).
Hii nchi ya kipekee duniani, hakukuwa na maombolezo rasmi na hadi leo matanga yanaendelea, mirathi yake ni migogogro mitupu. Wanaojaribu kudai Haki za nchi hii huandamwa na mauzauza ya walioiangamiza na wanaweza kupatwa na mabaya yasiyomithilika au kupotelea Kule ilikoenda nchi yao.
Watoto na wajukuu Wa nchi hii iliyofishwa wanagombana wenyewe kwa wenyewe hata kwenye kuandika muhtasari wa mustakabali wa Taifa lao na Sasa wanatawaliwa toka ng'ambo(Bahari kuu) na hawana mbinu za kujiasua.
Jambo hili linahitaji nguvu na akili ya ziada ili kuliweka sawa. Tufukue kaburi maana taarifa za kitaalam zinaonyesha kwa uhakika hajafariki maana tunaona mtikisiko chini ya Ardhi anavyopumua kwa taabu, tusipofanya hima atafariki rasmi muda si mrefu ujao.
Tujadili.