Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ex wakeYeye anaweza akawa kivuli tu maamuzi yote yanatoka kwa mstaafu
Historia ya kupikwa ikafunzwa katika skuli zetu,Tanganyika ikazikwa bila maombolezo na jina lake likafanywa kuwa chukizo masikioni mwa watu.Kosa kubwa linalofanyika hivi sasa hapa nchini ni kurithi makosa ya kuitawala yaliyofanyika hapo kabla, na hatimaye sasa kuyachukilia kama ndiyo miiko sahihi inayopaswa kufuatwa. Makosa hayo yamepelekea watu wengi kufungwa katika nira ya kutoweza kufikiria nje ya kasha.
Kuna kosa la kwanza litokanalo na kubinafsisha historia ya mapambano ya uhuru na kuyahusisha na watu wawili tu. Ijapkuwa kuna watu wengi sana ambao nyuma yao ipo sehemu muhimu ya historia kupitia michango yao ya kujitoa kwa hali na mali, bado ushiriki wao wala hautambuliwi, na pengine unafichwa kwa makusudi ili historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ubaki kuwa alama ya watu wawili, na kwa faida ya vyama vya TANU na ASP ambavyo ni wazazi wa CCM.
Wakati historia ikimpamba Nyerere kuwa ndiye mwamba pekee dhidi ya utawala wa kikoloni na kupeleka kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. Kwa upande wa Zanzibar, historia inampamba Karume kuwa ndiye alama kuu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kosa la pili ni hili la muundo wa JMT. Mchakato mzima ulioileta serikali ya JMT ulitawaliwa na kasoro nyingi sana. Ni ukweli usiotia shaka kuwa muundo huu ulikuwa ni kama ule wa mchezo wa utotoni;
"Sanda kalawe, Amina! Mwenye kupata, Apate! Mwenye kukosa, Akose!"
Na kwa hakika ndivyo ilivyokuwa, Nyerere akaambulia urais wa serikali kuu ya JMT, na ili kumpooza wenzake akampasa kubakia na urais wake wa serikali ya Zanzibar, na hapo ndipo mwili wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika ulopizikwa rasmi.
Badala ya kutambua uwepo wa serikali mbili zinazounda muungano na ziongozwe na mawaziri wakuu, na kisha itafutwe serikali kuu ambayo ingeongozwa na Rais wa JMT. Ubinafsi wa kutaka kuvitambua vya TANU na ASP kama sehemu pekee ya historia ya uhuru, na tamaa ya kugawana vyeo ndiyo ikapelekea kifo cha mpendwa wetu Tanganyika.