dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
kumbukumbu inayofanyika Jijini Kigali na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Ulaya, Amerika na Asia wakiongozwa na Rais Paul Kagame.
Ishara ya kuanza kwa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ni pamoja na kuwashwa kwa mishumaa katika eneo la Gisozi mahala ambapo mabaki ya miili ya watu zaidi ya 250,000 imezikwa katika kaburi la pamoja.
Mauaji hayo ya kimbari yalianza April 7, 1994 siku moja baada ya Ndege iliyombeba Rais wa wakati huo Juvenali Habyarimana na aliyekuwa Rais wa Burundi Cyprian Ntaryamira kudunguliwa wakati ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kigali.
Baada ya tukio hilo majeshi ya serikali ya wakati huo na makundi yenye silaha ya Impunzamugambi na Intarahamwe yaliyokuwa na unasaba na chama tawala MRND yalianza kuwaua watu wa Jamii ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani.
✍🏿 @fredricknwaka
🎤 @e_j1official