Nchi yazizima ushindi wa CCM maelfu wajitokeza mitaani kushangilia

nzagambadume

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
2,430
Reaction score
5,787
Amini usiamini, ni kishindo cha nzima na dunia nzima imetikisika baada ya ushindi wa kishindo wa kile chama kikongwe duniani kinachofanya siasa zake kwa njia za kisasa yaani za kisayansi chini ya magwiji ya kisiasa kama daud bashite, mzee polepole na Bashiru

Melefu ya wanyonge ambao maisha yao yameboreshwa kwa kasi katika awamu hii ya tano wamejitokeza barabarani kwa wingi kushangilia ushindi huo wa kishindo dhidi ya VIBARAKA WA MABEBERU ambao walishindwa hata kujaza fomu
Pongezi za dhati pia zimetolewa kwa WAZALENDO WAPENDA AMANI a.k.a watendaji wa kata na wakurugenzi kwa kuwaengua VIBARAKA WA MABEBERU ambao lengo lao ni kuleta machafuko nchini ili waondoe amani amabayo imeletwa na ccm huku ikitunzwa na jeshi mahiri kabisa la polisi barani afrika yaani police tz

Hii hapa chini ni mojawapo ya video zinazoonyesha shamrashamra hizo za kihistoria kabisa

Hasa mwenyekiti wao wa taifa alivyo handsome!!! Hadi mrembo toka kisarawe kalegea na kujilengesha!!

Chama juu, juu zaidi!
 
Hahahaha Mkuu yaani nimecheka sana kwa kweli,kuwa mwanachama wa CCM inahitaji moyo mgumu zaidi ya paka na kutokubali kutumia akili kabisa!!..
FB_IMG_1574154869610.jpeg
 
Aisee kweli CCM inatisha, wananchi wamejaa na kuishangilia sana kwa ushindi waliopata
 
sasa si mmeweka mpira kwapani acha tushangilie mngeaibika sanaaaaaaaaaa
 
Hakuna ushindi bila ushindani na pia hakuna ufaulu usopimwa kwa mitihani hiyo ndo kanuni ktk siasa za ushindani.
 
Amini usiamini, ni kishindo cha nzima na dunia nzima imetikisika baada ya ushindi wa kishindo wa kile chama kikongwe duniani kinachofanya siasa zake kwa njia za kisasa yaani za kisayansi chini ya magwiji ya kisiasa kama daud bashite, mzee polepole na Bashiru

Melefu ya wanyonge ambao maisha yao yameboreshwa kwa kasi katika awamu hii ya tano wamejitokeza barabarani kwa wingi kushangilia ushindi huo wa kishindo dhidi ya VIBARAKA WA MABEBERU ambao walishindwa hata kujaza fomu
Pongezi za dhati pia zimetolewa kwa WAZALENDO WAPENDA AMANI a.k.a watendaji wa kata na wakurugenzi kwa kuwaengua VIBARAKA WA MABEBERU ambao lengo lao ni kuleta machafuko nchini ili waondoe amani amabayo imeletwa na ccm huku ikitunzwa na jeshi mahiri kabisa la polisi barani afrika yaani police tz

Hii hapa chini ni mojawapo ya video zinazoonyesha shamrashamra hizo za kihistoria kabisa

Waache washangilie, hata Unguja baada ya kupora walishangilia.
 
Back
Top Bottom