DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Singida, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Theresia Mdendemi, amesema kwamba maendeleo ya nchi hayawezi kufikiwa bila uwepo wa amani, utulivu na usalama. Alieleza kuwa hali hiyo huwapa wananchi nafasi ya kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi bila bugudha.
Ameyasema hayo Oktoba 19, 2025 alipokuwa akitoa elimu ya ulinzi na usalama kwa waumini wa Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu lililopo Makao Makuu ya Jimbo Katoliki Singida, Kata ya Mughanga, Tarafa ya Mungumaji, Manispaa ya Singida. Katika ujumbe wake, aliwaasa waumini hao kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, hasa katika kipindi cha uchaguzi.
ASP Mdendemi aliwahakikishia waumini hao kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kulinda usalama wa wananchi na mali zao wakati wote, ikiwemo kipindi cha uchaguzi. Pia aliwasihi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili wa kijinsia au unyanyasaji dhidi ya watoto, badala ya kujichukulia sheria mkononi.