Kamwe hatuwezi kushindana na nchi zilizoendelea kiviwanda, bila kuwa na sera ya kuvilinda viwanda vyetu, kama ni mfuatiliaji wa historia ya maendeleo ya viwanda duniani, utakumbuka kwamba Uingereza ndiyo nchi ya kwanza duniani kuwa na viwanda vya nguo vingi, na ili kuvilinda dhidi ya viwanda vingine, Uingereza ilipiga marufuku na kuzuia uzalishaji wa nguo duniani kote, hasa katika nchi alizokua anazitawala, sana sana India ili aweze kuuza nguo zake tu, japo nchi hizo hazikuwa na technolojia bora zaidi ya Uingereza, hadi leo Marekani inapambana kulinda soko lake la magari dhidi ya magari ya Japan.
Mbona unazungumzia eneo moja pekee la bei ya nguo lakini hayo mengine yote kuhusu uchumi mpana unaotokana na viwanda huzungumzii?, unadhani nchi hii itaendelea kwa kutegemea kuagiza bidhaa pekee toka nje ya nchi bila kujitahidi kutengeneza vitu vyetu?. Kama tutafuata unavyosema wewe basi tuagize kila kitu toka nje, kwasababu karibu vitu vyote vya nje vina bei nafuu na ni bora ukilinganisha na hapa nchini.