Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Nchi za Kiarabu muda wa kuishinda Israel ni sasa

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Viongozi wa nchi za kiislamu wasijitumbukize katika ujinga utakaowagharimu dunia na akhera yao.Kama ni maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu Palestina yapo makumi kadhaa na hayajatekelezwa hata moja.Kinyume chake maazimio hayo yanavunjwa mbele ya macho yao.

Anthony Blinken ameitembelea Israel kuipa pole kutokana na mashambulizi ya Hamas kwenye ardhi zao.Sambamba na yeye ndege za mizigo zimekuwa zikipeleka shehena kubwa za silaha nchini Israel ambayo tangu hapo haina upungufu wa vifaa hivyo.

Sambamba na hilo tena meli kubwa ya kivita na ya kisasa kuliko zote imeshapelekwa jirani kabisa na Gaza na karibu na Israel.Meli hiyo kwa ukubwa wake na vifaa vilivyomo na idadi ya askari wanaokuwemo humo ni sawa na kusema kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani imesogezwa karibu kuisaidia Israel kuimaliza Palestina.

Wakati wa press conference hapo jana kati ya Blinken na Netanyahu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani alitaja udugu alionao na Israel.Katika kuomboleza vifo vya raia wa Israel alitokwa na machozi katikati ya hotuba yake.

Baada ya kuondoka hapo imeelezwa ratiba inaonesha ataendelea na ziara kuzitembelea Jordan,Misri na Saudi Arabia.

Nini anakwenda kuwaambia nchi hizo. Huku muda huo huo Israel inaongeza ukatili wake kwa wapalestina ikitaka watu milioni moja na ushei wahame makazi yao katika kipindi cha masaa 24. Pamoja na kwamba haiwezekani kwa muda huo watu idadi hiyo kuhama pia huko wanakoelezwa waende hakuna mazingira ya kuwapokea. Kote ni kifo tu. Watakaoshindwa kuhama watakapouliwa itatolewa sababu kuwa waliambiwa wahame. Kule wanakotakiwa kwenda hakuna nyumba,maji ,chakula na umeme na bado hakuna uhakika kuwa hawatadondoshewa mabomu.

Kama ni udugu uliomliza Blinken kwa ndugu zake Israel,jee waislamu na waarabu hawana udugu ulio bora zaidi na wenzao wa Palestina.Waislamu wakizidi kuwa wajinga watamalizwa kabisa.

1697175757773.png
 
Kwa mfano ww ndio Dubai..ungefanyaje? Wakati wanaoingiza dola nyingi nchini kwako ni wazungu
Faida za dola ni ndogo kuliko faida ya kulinda roho za ndugu zako.
Hata hivyo pale Dubai wazungu katika serikali ni wengi kuliko waarabu.Hivyo hiyo mamlaka ya kuzuia hawana.Ni aina ya ujinga wao kwa kuipenda dunia.
 
Faida za dola ni ndogo kuliko faida ya kulinda roho za ndugu zako.
Hata hivyo pale Dubai wazungu katika serikali ni wengi kuliko waarabu.Hivyo hiyo mamlaka ya kuzuia hawana.Ni aina ya ujinga wao kwa kuipenda dunia.
ndugu ambao hukushambulia muda mwingine?
 
kwa hili waliloanza fanya hamas bas ukiendelea kushabikia ww ni kichaa
Ukiangalia kote duniani wanaoiunga mkono Hamas wamekuwa ni wengi kuliko wanaoilaumu kama wewe.Nchi kama Ufaransa imebidi ipige marufuku maandamano ya kuipongeza Hamas. Na Ujerumani mpaka kuna viongozi wa Marekani wameilaumu kwa kuwa na maandamano makubwa ya kuiunga mkono Hamas
 
Hizo meli na ndege za kivita za Marekani hazikuenda kwa ajili ya kupigana na kakikundi kalikowatoa jasho waisrael bali ni hofu kwa Iran na Edrogan
Hivi kweli meli hiyo ya Gerald Ford na nyingine ambayo iko njiani ya USS Abraham Lincoln kwa ajili ya Hamas hapana
 
Back
Top Bottom