Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Viongozi wa nchi za kiarabu waliokutana huko Cairo wamesema Gaza itajengwa kwa plani nzuri waliyokwisha kuibuni wakati wapalestina hao wakiwa humo humo ndani.
Raisi Elsisi ambaye mara nyingi ameonekana kama kibaraka mkubwa wa Marekani ameongoza kwa kutoa tamko kali akisema zaidi ya kuijenga Gaza wanataka kuona taifa la Palestina likiundwa haraka japo iwe sambamba na kubaki kwa Israel.
Waarabu hao wamesema watachangia jumla ya dola bilioni 53 kwa kazi hiyo itakayokuwa na awamu tatu muhimu.
Ya kwanza ni kuwaingiza wapalestina kwenye mahema na nyumba za kontena haraka iwezekanavyo na ifuatiwe na kusafishwa kifusi pamoja na kufyatua mabomu yaliyobaki ndani ya Gaza ambayo hayakuripuka