Nchi za magharibi haziamini tena juu ya Free Market?

Nchi za magharibi haziamini tena juu ya Free Market?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Ni rahisi sana kuhubiri kuhusu free market (Biashara Huria) iwapo upo kwenye advantage. Lakini ukiwa unajitafuta biashara huria ni ugonjwa mbaya sana. Nchi za magharibi zimehubiri sana kuhusu biashara huria. Watu wafanye biashara na bidhaa zizunguke duniani bila vikwazo. Ikafika hadi nchi maskini tukaaminishwa kuwa biashara huria ni nzuri hata kwetu, na tukaamini.

Leo hii China ndiyo yupo kwenye advantage ya kuzalisha na kuuza duniani. Nchi za magharibi zimeanza kuona machungu ya biashara huria. Kazi za uzalishaji zinakufa na ajira zinapotea sababu bidhaa zao haziwezi kushindana na za China. Sasa wameanza figisu dhidi ya China.

Wanamuandama mchina kwenye kila sekta ya biashara. Sehemu moja ni kwenye magari ya umeme. China amejipanga sana kwenye hii sekta. Inaongoza kwenye kila nyanja inayohusu magari ya umeme. Nchi za magharibi haziwezi kabisa kushindana naye.

Biashara huria waliyokuwa wanahubiri imerudi kuwatafuna. Wameamua kupambana naye kwa kumuwekea vikwazo magari yake ya umeme yasiingie nchi zao kirahisi. Wanayapiga kodi kubwa huku wakitoa visingizio kibao.

Wanakataa bidhaa za pamba kutoka China zisiingie nchi zao kwa kisingizio kuwa zinalimwa na Uighurs wanaokandamizwa. Piga ban Huawei, Tik Tok kwa visingizio kibao(Japo China nao wameban makampuni ya tech ya magharibi).

Nchi za magharibi zimeishauona ubaya wa soko huria?
 
Protectionism.
The policy of imposing duties or quotas on imports in order to protect home industries from overseas competition

Ndicho West wanachofanya kwa sasa
Na ukweli ukitaka kukuza viwanda vya ndani lazima ufanye protectionism kwanza. Nchi za magharibi kabla hazijawa juu zilifanya sana protectionism. Baada ya kuona sasa hakuna wa kushindana nao wakaanza kuhubiri soko huria. Leo wanaona hawako vizuri wanaanza kurudi kwenye protectionism polepole.
 
Uchumi wa Marekani kwa sasa unafanya vizuri, hizo story za ajira zimepotea sijui umezitoa wapi wakati unemployment rate ni 4% tu
Ajira za service industry. Kuuza migahawa. Ajira za kuexport zimekufa. Raisi wao mmoja alisema kuwa nchi haiwezi kuendelea kwa wao kuuziana vyakula na kupakiana nyumba rangi wao kwa wao. Lazima waexport.
 
Protectionism.
The policy of imposing duties or quotas on imports in order to protect home industries from overseas competition

Ndicho West wanachofanya kwa sasa
Protectionism ni sehemu ya free market,
Kinyume cha free market ni command economy.
 
Inapokuwa one way siyo soko huria tena inakuwa sera ya kulinda viwanda vya ndani
Usichanganye soko huria na globalisation, soko huria linaweza kuwa la ndani ya nchi tu, la kikanda, la kibara au la kidunia. Nchi husika ndio inaamua ukubwa wa soko lake huria, pia nchi inaweza kukataa au kuweka vikwazo vya kufanya biashara na nchi nyingine kwa sababu nyingi na ikabaki kuwa ni free market economy na kwa mantiki hiyo US ni free market economy hata kama imepiga marufuku biashara na Iran, Cuba Venezuela, Korea Kaskazini na Urusi.
 
Ajira za service industry. Kuuza migahawa. Ajira za kuexport zimekufa. Raisi wao mmoja alisema kuwa nchi haiwezi kuendelea kwa wao kuuziana vyakula na kupakiana nyumba rangi wao kwa wao. Lazima waexport.
US ndio nchi namba mbili kwa exports duniani baada ya China. US wana exports za $Trillion 3 kwa mwaka wakiwafuatia China wenye exports $Trillion 3.5
 
Usichanganye soko huria na globalisation, soko huria linaweza kuwa la ndani ya nchi tu, la kikanda, la kibara au la kidunia. Nchi husika ndio inaamua ukubwa wa soko huria, pia nchi inaweza kukataa au kuweka vikwazao vya kufanya biashara na nchi nyingine kwa sababu nyingi na ikabaki kuwa ni free market economy kwa mantiki hiyo US ni free market economy hata kama imepiga marufuku biashara na Iran, Venezuela, Korea Kaskazini na Urusi.
Kwenye free market bei inaamuliwa na demand na supply. Kama US anaweza kuchezesha bei ya mafuta na gesi kwa kuwawekea vikwazo Urusi, Venezuela na Iran hiyo siyo free market. Kama anachezesha bei ya magari ya umeme kwa kuweka kodi kubwa kwa magari ya China, kodi ambazo hata WTO hawakubaliani nazo hiyo si free market.
 
Na ukweli ukitaka kukuza viwanda vya ndani lazima ufanye protectionism kwanza. Nchi za magharibi kabla hazijawa juu zilifanya sana protectionism. Baada ya kuona sasa hakuna wa kushindana nao wakaanza kuhubiri soko huria. Leo wanaona hawako vizuri wanaanza kurudi kwenye protectionism polepole.
Mapinduzi ya viwanda yalianzia nchi za magharibi sasa hizo Protectionism za viwanda walifanya dhidi ya nani asiye wa magharibi??
 
Kwenye free market bei inaamuliwa na demand na supply. Kama US anaweza kuchezesha bei ya mafuta na gesi kwa kuwawekea vikwazo Urusi, Venezuela na Iran hiyo siyo free market. Kama anachezesha bei ya magari ya umeme kwa kuweka kodi kubwa kwa magari ya China, kodi ambazo hata WTO hawakubaliani nazo hiyo si free market.
Siku ukifika mahakamani ndio utajua tofauti ya manslaughter na murder, pia kodi ni sehemu ya free market, kila taifa linaamua ukubwa wa kodi zake kwa sababu zake, WTO walitakiwa wawaambie serikali ya Wakomunisti China kwanza wasiwe wanafanya devaluation ya currency yao ili ku boost exports zao.
 
US ndio nchi namba mbili kwa exports duniani baada ya China. US wana exports za $Trillion 3 kwa mwaka wakiwafuatia China wenye exports $Trillion 3.5
Pamoja na hilo bado wana trade deficit. Kuwa na trade surplus ni muhimu kuliko ukubwa wa export yako. Hizo tariffs zote dhidi ya bidhaa za China ni katika kupambana na trade deficit. Nchi karibu zote za magharibi zinakabiliwa na hatari ya trade deficit.
 
Mapinduzi ya viwanda yalianzia nchi za magharibi sasa hizo Protectionism za viwanda walifanya dhidi ya nani asiye wa magharibi??
Mfano mmoja. Waingereza walikuwa wanakataa kuwauzia Waholanzi sufi. Waholanzi walikuwa na viwanda bora san vya nguo. Uingereza wao walikuwa na kondoo wa sufi wazuri ila hawana viwanda bora vya nguo hivyo walikuwa wanaexport sufi kwenda Uholanzi. Ili kukuza viwanda vyao vya nguo wakapiga ban kuexport sufi kwenda Uholanzi.
Uingereza ilipoitawala India ilipiga marufuku uanzishwaji wa viwanda vya nguo India ili kulinda viwanda vyao nyumbani.
 
Siku ukifika mahakamani ndio utajua tofauti ya manslaughter na murder, pia kodi ni sehemu ya free market, kila taifa linaamua ukubwa wa kodi zake kwa sababu zake, WTO walitakiwa wawaambie serikali ya Wakomunisti China kwanza wasiwe wanafanya devaluation ya currency yao ili ku boost exports zao.
Hakuna anayesema kwenye free market hakuna kodi. Lakini lengo la kodi ni mapato na si kucontrol bei ya bidhaa.
 
Back
Top Bottom