kwa-muda
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 2,097
- 5,348
mchina anazidi kuipiga kwenye mshono.... Nmeona kuwa UAE imeamua kununua ndege za kivita za kichina za j1-20 badala ya F-35 ya mmarekani.Ni rahisi sana kuhubiri kuhusu free market (Biashara Huria) iwapo upo kwenye advantage. Lakini ukiwa unajitafuta biashara huria ni ugonjwa mbaya sana. Nchi za magharibi zimehubiri sana kuhusu biashara huria. Watu wafanye biashara na bidhaa zizunguke duniani bila vikwazo. Ikafika hadi nchi maskini tukaaminishwa kuwa biashara huria ni nzuri hata kwetu, na tukaamini.
Leo hii China ndiyo yupo kwenye advantage ya kuzalisha na kuuza duniani. Nchi za magharibi zimeanza kuona machungu ya biashara huria. Kazi za uzalishaji zinakufa na ajira zinapotea sababu bidhaa zao haziwezi kushindana na za China. Sasa wameanza figisu dhidi ya China.
Wanamuandama mchina kwenye kila sekta ya biashara. Sehemu moja ni kwenye magari ya umeme. China amejipanga sana kwenye hii sekta. Inaongoza kwenye kila nyanja inayohusu magari ya umeme. Nchi za magharibi haziwezi kabisa kushindana naye.
Biashara huria waliyokuwa wanahubiri imerudi kuwatafuna. Wameamua kupambana naye kwa kumuwekea vikwazo magari yake ya umeme yasiingie nchi zao kirahisi. Wanayapiga kodi kubwa huku wakitoa visingizio kibao.
Wanakataa bidhaa za pamba kutoka China zisiingie nchi zao kwa kisingizio kuwa zinalimwa na Uighurs wanaokandamizwa. Piga ban Huawei, Tik Tok kwa visingizio kibao(Japo China nao wameban makampuni ya tech ya magharibi).
Nchi za magharibi zimeishauona ubaya wa soko huria?
yani anakaba kila kona. Umoja wa Ulaya wanahaha hadi nimeona wanasema ili kuweza kushindana na mchina wanapaswa kila mwaka watumie sijui euro bilioni 800 kwa ajili ya uwekezaji nazo haijulikani zinatoka wapi.
Yani mchina kageuka zimwi sasa hivi. Kampuni za magari kama VW na Benz wanaomba umoja wa ulaya ufikirie upya kuhusu vikwazo walivyoweka kwa gari za mchina maana mchina akijibu watapoteza soko kubwa pia maana mchina ni soko kubwa la magari yao.