Nchi za magharibi haziamini tena juu ya Free Market?

mchina anazidi kuipiga kwenye mshono.... Nmeona kuwa UAE imeamua kununua ndege za kivita za kichina za j1-20 badala ya F-35 ya mmarekani.
yani anakaba kila kona. Umoja wa Ulaya wanahaha hadi nimeona wanasema ili kuweza kushindana na mchina wanapaswa kila mwaka watumie sijui euro bilioni 800 kwa ajili ya uwekezaji nazo haijulikani zinatoka wapi.
Yani mchina kageuka zimwi sasa hivi. Kampuni za magari kama VW na Benz wanaomba umoja wa ulaya ufikirie upya kuhusu vikwazo walivyoweka kwa gari za mchina maana mchina akijibu watapoteza soko kubwa pia maana mchina ni soko kubwa la magari yao.
 
Hujamaliza moja unarukia lingine, kaa sehemu moja utulie. Umesema export sector ya Marekani imekufa na kwamba wamebaki na uchumi wa vinyozi na mama ntilie n.k nimekuonyesha hapo wao ni namba 2 kwa exports duniani umerukia mambo ya trade deficit!
 
Wakipiga Pini pamba Tanzania lazima kitulambe maana mzigo mwingi unaenda china
 
Hakuna anayesema kwenye free market hakuna kodi. Lakini lengo la kodi ni mapato na si kucontrol bei ya bidhaa.
Sio kila bidhaa ina maslahi kwa nchi, kama nchi inatumia pesa nyingi kutibu majeruhi watokanao na ajali za pikipiki na inapoteza nguvu kazi kubwa ya vijana kupitia ajali za pikipiki suluhisho mojawapo ni kuongeza kodi za pikipiki ili vijana wakafanye kazi nyingine tofauti na bodaboda na pia hizo kodi zikajenge hospital nyingi zaidi na kuajiri madaktari wengi.

Pia control ya bei sio tatizo wala haiiondoi nchi katika free market economy, kodi yoyote ile tayari ni kuingilia bei iwe kwa kukusudia au kutokusudia hivyo, mjadala mkubwa ni jinsi gani hiyo control inafanyika, kwa sababu zipi, kwa maslahi ya nani, kwa ukubwa gani na kwa ufanisi gani. Katika free market economy kuna "welfare capitalism" pia
 
Siyo kinyume sema mbadala wa soko huria ni πŸ‘‰ Strategic market hapa ndipo wazungu wao wana cheza huku wakiwaambia wapumbavu wa ccm wafanye soko huria
Hamuwezi hata kununua bidhaa za Wazungu. Bidhaa zote mnanunua China, mafuta mnanuna uarabuni. Softwares hamuwezi kuunda kwa hiyo hamna namna ila kuendelea kutumia Microsoft, twitter, Android, WhatsApp n.k. Watalii wazungu bado mnategemea pesa zao sasa hata msipoambiwa muwe na soko huria mna mbadala gani??
 
Umesoma nilicho andika au? Nimekuambia mbadala ni soko la kimkakati (strategic market)
 
Kodi inazopigwa china ni za protectionism
 
Inahitajika nguvu nyingi kutetea kodi ya Chinese EVs ndani ya Marekani. Justification yake ni ndogo sana, ni kupunguza ushindani kwa nguvu ya kodi.

Tofauti ya nchi za Afrika ni kuwa wajinga wakurupukaji wa mifumo ya kidunia ambayo haina maslahi kwake. Wakati wazungu mfumo ukishaenda kinyume nao wanatafuta alternative au visingizio.
 
Kodi inazopigwa china ni za protectionism
US wana sera za protectionism katika uhai wake wote kama taifa, hizo tariffs kwa Wachina ni sehemu mojawapo tu na hazijaanza leo, US wamekuwa wanawapa wakulima wao (ruzuku)subsidies, wanadhibiti intellectual property rights za watu wake, serikali inadhibiti pakubwa mauzo ya silaha muhimu nje ya nchi n.k sasa sijui kwa nini hao Wachina kuwekwa tariffs tu leo hii ndio iifanye US kutokuwa free market economy!

Nchi inaweza kuwa free market economy bila kuwa na free trade.
 
Wakitubana Sisi halali yao, sasa wamebanwa na china imekuwa haramu .
 
US ndio nchi namba mbili kwa exports duniani baada ya China. US wana exports za $Trillion 3 kwa mwaka wakiwafuatia China wenye exports $Trillion 3.5
Hii imekaaje wa kwanza awekwa wa mwisho. tangu sasa hufai kua mchambuzi wa haya mambo tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…