Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na changamoto mbalimbali, mzigo wa madeni wa nchi za Afrika umeongezeka. Baadhi ya nchi za magharibi zinadai kuwa China ndio inaibebesha Afrika “mtego wa madeni”. Lakini ukweli ni kwamba, nchi hizo ndio wahusika wakuu wa mzigo wa madeni wa Afrika.
Katika muda mrefu uliopita, mikopo ya China kwa Afrika imetumika zaidi katika ujenzi wa miundombinu, na nchi za Afrika zinaona kwamba mikopo ya China inazisaidia kuongeza uwezo wa kujiendeleza, kuboresha maisha ya watu, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa Afrika. Kuhusu suala la ulipaji wa madeni, China imesaini makubaliano ya kuchelewesha ulipaji madeni na nchi 19 za Afrika, na kuwa nchi inayoruhusu kuchelewesha ulipaji madeni mengi zaidi kwa Afrika kati ya nchi wanachama wa Kundi la Nchi 20 (G20). Hivi majuzi, China ilitangaza kuwa itasamehe mikopo 23 bila ya riba ya nchi 17 za Afrika iliyopaswa kulipwa kufikia mwisho wa 2021.
Tukichunguza chanzo cha mzigo wa madeni barani Afrika, Marekani na baadhi ya nchi nyingine za Magharibi ndio wahusika wa kweli. Ripoti zinazochambua madeni ya Afrika zilizotolewa hivi karibuni zimedhihirisha kuwa, benki za nchi za Magharibi na wakopeshaji wa kibinafsi ndizo zimeleta mzigo mkubwa wa madeni kwa Afrika.
Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, kati ya madeni ya nje ya jumla ya dola bilioni 696 za Kimarekani ya nchi 49 za Afrika, robo tatu zimekopwa kutoka mashirika ya kimataifa ya fedha na mashirika ya kibinafsi yasiyo ya China. Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza inaonyesha kuwa, wakopeshaji wa nchi za Magharibi ni chanzo kikuu cha madeni ya nje barani Afrika. Wakati huo huo, ripoti iliyotolewa na Shirika la Misaada la Uingereza “Debt Justice” inaonesha kuwa, asilimia 35 ya madeni ya nje ya nchi za Afrika yanatoka kwa wakopeshaji binafsi wa Magharibi, na kiasi hicho ni karibu mara tatu ya mikopo ya China kwa Afrika, na wastani wa riba ni takriban mara mbili ikilinganishwa na ile inayotolewa na China.
Hata hivyo, wakopeshaji wa Magharibi wanakataa kushiriki katika mpango wa kuchelewesha ulipaji madeni ya Afrika uliopendekezwa na G20, na hali hii imezifanya nchi za Afrika zikabiliwe na wakati mgumu zaidi.
Aidha, ikilinganishwa na mikopo ya China kwa Afrika, mikopo kutoka kwa nchi za Magharibi inatumika zaidi katika maeneo yasiyo ya uzalishaji na maendeleo, ambayo ni vigumu kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa kujiendeleza. Zaidi ya hayo, nchi za Magharibi pia zimeweka masharti mbalimbali wakati wa kutoa mikopo kwa nchi za Afrika, ili kuathiri mambo ya kisasa ya nchi hizo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sera za Afrika ya Kenya Peter Kagwanja alisema: “Marekani na nchi nyingine za Magharibi zina mikopo mingi zaidi barani Afrika, na viwango vya riba ni vya juu kuliko China. Zinaogopa kwamba nchi za Afrika zitapata fedha na rasilimali zinazohitajika kutoka upande mwingine, hivyo zinaipaka matope China na kusema, China inafanya ‘diplomasia ya madeni’ na ‘ukoloni mamboleo’ barani Afrika.” Hata hivyo, ukweli umeonyesha kuwa ni Marekani na nchi za Magharibi ambazo zimeweka mtego wa madeni barani Afrika.