Nchi zenye wakimbizi wengi hatarini kupata maambukizi makubwa ya Corona, Tanzania yatajwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
CtmcM5vWgAA9Kcd-620x309.jpg
Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge Kenya
NCHI ambazo zinahifadhi wakimbizi wengi na zenye makazi duni Afrika, zinatajwa kuwa na hatari zaidi ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) katika siku za usoni.
Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge nchini Kenya, ametaja nchi ambazo iwapo hatua kali hazitachukuliwa, zinaweza kujikuta kwenye hatari zaidi ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania.
Na kwamba, nchi hizo baadhi zina idadi kubwa ya wakimbizi ambao wamewekwa pamoja, lakini pia yapo maeneo wakazi wake wamefungamana na kuwa hatari zaidi katika kuenea kwa ugonjwa huo ikiwemo Kibera, Kenya.

Pia amesema, maeneo yaliyo na vita na majanga mengine ikiwemo Sudani Kusini, yamo kwenye hatari kubwa ya ugonjwa huo, hivyo akishauri hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukabili virusi hivyo.

“Nchi zilizo katika Jangwa la Saharan, kwa sasa zina kesi za maambukizi zaidi ya watu 1,300 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
“Hasa nchi ambazo zinahifadhi wafungwa wengi na makazi duni ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania,” anasema.

Katika taarifa yake aliyoitoa tarehe 25 Machi 2020, Derbyshire anasema, mji wa kibera uliojitenga, una hatari zaidi kutokana na mazingira yake duni yanayotokana na kukosa maji safi, sabuni na vituo bora vya afya.

“Tumeona namna ambavyo nchi zilizoendelea kwa kiwango kikubwa katika masuala ya afya, zinataabika. Ni rahisi kujua sasa kwa kiwango gani corona inavyoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha janga duniani, wazee ndio wanaotaabika sana,” amesema Derbyshire.

Anasema, watu wenye umri mkubwa ndio wameathirika sana na corona, na wameathirika zaidi kutokana na kinga zao kuwa na uwezo mdodogo – dhaifu.
Hivyo amesema, hatari zaidi ni kwa watu wenye umri mkubwa wanaoishi katika mazingira magumu ya upatikanaji hafifu wa chakula, maji na huduma za afya.
 
W
CtmcM5vWgAA9Kcd-620x309.jpg
Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge Kenya
NCHI ambazo zinahifadhi wakimbizi wengi na zenye makazi duni Afrika, zinatajwa kuwa na hatari zaidi ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) katika siku za usoni.

Na kwamba, nchi hizo baadhi zina idadi kubwa ya wakimbizi ambao wamewekwa pamoja, lakini pia yapo maeneo wakazi wake wamefungamana na kuwa hatari zaidi katika kuenea kwa ugonjwa huo ikiwemo Kibera, Kenya.

Pia amesema, maeneo yaliyo na vita na majanga mengine ikiwemo Sudani Kusini, yamo kwenye hatari kubwa ya ugonjwa huo, hivyo akishauri hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukabili virusi hivyo.

“Nchi zilizo katika Jangwa la Saharan, kwa sasa zina kesi za maambukizi zaidi ya watu 1,300 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
“Hasa nchi ambazo zinahifadhi wafungwa wengi na makazi duni ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania,” anasema.

Katika taarifa yake aliyoitoa tarehe 25 Machi 2020, Derbyshire anasema, mji wa kibera uliojitenga, una hatari zaidi kutokana na mazingira yake duni yanayotokana na kukosa maji safi, sabuni na vituo bora vya afya.

“Tumeona namna ambavyo nchi zilizoendelea kwa kiwango kikubwa katika masuala ya afya, zinataabika. Ni rahisi kujua sasa kwa kiwango gani corona inavyoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha janga duniani, wazee ndio wanaotaabika sana,” amesema Derbyshire.

Anasema, watu wenye umri mkubwa ndio wameathirika sana na corona, na wameathirika zaidi kutokana na kinga zao kuwa na uwezo mdodogo – dhaifu.
Hivyo amesema, hatari zaidi ni kwa watu wenye umri mkubwa wanaoishi katika mazingira magumu ya upatikanaji hafifu wa chakula, maji na huduma za afya.
WEMA TULIOWAFANYIA MAJIRANI, HUENDA IKAWA NI SABABU YA MUUMBA KUTUONEA HURUMA TUKA SAVAIVU KORONA.
 
Mungu anaendelea kutupigania,pamoja na takwimu zao wanazotupachika,bado hakuna kitisho.
 
Duh...!. Hivyo kufuatia Corona, nchi zote zenye migogoro inayotengeneza wakimbizi, isimamishe hostilities, tu deal na Corona kwanza kwa kuwawahisha wakimbizi kuwarejesha kwao fasta, kwasababu walikimbilia kwetu kujiokoa maisha, tusije kuwaua kwa Corona.

Corona ikiisha, hostilities ziendelee, tutawapokea tena.
P
 
Gia nyengine yatutisha, Mungu yupo atatutetea tu na takwimu zenu zitaisha kwa makaratasi huku tukiendelea kumtukuza Mungu mwenye rehema na fadhili zake za milele.
 
Kwani ye ni afisa wa WHO?? Muongo huyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Anarudia ngojera zile zile za Bill Gates, hawa watu ni maprophets of doom - wakuja kuhabika sooner or later, God willing.

Juzi hapa nilishangaa sana Bill Gates aliposema anajifungia ndani huko Seatle akihofia Coronavirus, yaani hakutegemea ugonjwa huu ungehikumba USA vile vile ndio maana alifikia hatua ya kuitabiria vibaya Africa alisema, na hapa namnukuu "Corona itahangamiza mamia ya mamillion ya Waafrica in Sub Sahara Africa!! Je, hivi sasa nini kinaendelea nchini mwake mpaka anafikia hatua ya yeye na mkewe kujifungia ndani.
 
Anatafuta huruma ya wafadhili ili apate fungu la 'Corona' kwa ajili ya Afrika litakalotoka soon.
CtmcM5vWgAA9Kcd-620x309.jpg
Justin Derbyshire, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la HelpAge Kenya
NCHI ambazo zinahifadhi wakimbizi wengi na zenye makazi duni Afrika, zinatajwa kuwa na hatari zaidi ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) katika siku za usoni.

Na kwamba, nchi hizo baadhi zina idadi kubwa ya wakimbizi ambao wamewekwa pamoja, lakini pia yapo maeneo wakazi wake wamefungamana na kuwa hatari zaidi katika kuenea kwa ugonjwa huo ikiwemo Kibera, Kenya.

Pia amesema, maeneo yaliyo na vita na majanga mengine ikiwemo Sudani Kusini, yamo kwenye hatari kubwa ya ugonjwa huo, hivyo akishauri hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukabili virusi hivyo.

“Nchi zilizo katika Jangwa la Saharan, kwa sasa zina kesi za maambukizi zaidi ya watu 1,300 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
“Hasa nchi ambazo zinahifadhi wafungwa wengi na makazi duni ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Ethiopia na Tanzania,” anasema.

Katika taarifa yake aliyoitoa tarehe 25 Machi 2020, Derbyshire anasema, mji wa kibera uliojitenga, una hatari zaidi kutokana na mazingira yake duni yanayotokana na kukosa maji safi, sabuni na vituo bora vya afya.

“Tumeona namna ambavyo nchi zilizoendelea kwa kiwango kikubwa katika masuala ya afya, zinataabika. Ni rahisi kujua sasa kwa kiwango gani corona inavyoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha janga duniani, wazee ndio wanaotaabika sana,” amesema Derbyshire.

Anasema, watu wenye umri mkubwa ndio wameathirika sana na corona, na wameathirika zaidi kutokana na kinga zao kuwa na uwezo mdodogo – dhaifu.
Hivyo amesema, hatari zaidi ni kwa watu wenye umri mkubwa wanaoishi katika mazingira magumu ya upatikanaji hafifu wa chakula, maji na huduma za afya.
 
Tafiti uchwara,kwani huko ambako wanakufa kila siku kulikua na wakimbizi waliosongamana?
 
Back
Top Bottom