Nchi zetu zifanye kama Israel kuyasambaratisha makundi ya kigaidi huku akimpiga na mfadhiri wa makundi hayo!

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Makundi ya Kigaidi huwezi kuyamaliza kama hujadhoofisha nguvu ya mfadhili wao

Wengi tumeona vita vya Israel na makundi yaliyokuwa yakiisumbua nchi hiyo

IDF hakuwa akipiga wanamgambo tu wa makundi ya kigaidi, bali aliwapiga na wafadhili wao wakuu na kuwadhoofisha kabisa, pale alipopiga mitambo mingi ya kutengeneza siraha na hata mitambo ya kutengeneza mabomu, rada mbalimbali za kiulinzi kule Iran na Iran akaogopa na kukaa kimya

Nchi hizi zilizoungana kupambania Congo na kupigana na wanamgambo wa M23, kwa nini sasa zisitumie mbinu hii kushambulia moja kwa moja mfadhili wa kundi hilo?

Siku hizi wapiganaji hununuliwa kwa fedha, huwezi kulishinda kundi linalofadhiliwa na nchi ambayo iko na malengo katika hilo,

Ili kushinda makundi kama hayo, ni kumpiga mfahili wao

Na ama hakuna mpango huo, basi tuendelee kupokea maiti za watu wetu kizembe

Na itafika hatua hatutakubali kupelekwa wanajeshi wetu kwenye jambo ambalo halitupi faida kama nchi zetu,

Nazungumzia hasara kwa sababu tumeamua kuukwepa kuukata mziizi wa fitina

Apigwe mfadhili wa kundi la M23 na hakutakuwa na vita tena Congo

Mungu Ibariki Tanzania, na Mungu ibariki Africa
 
Congo igawanywe itoe nchi tatu au nne
Italeta Utulivu mkuu, maana mpaka sasa najua ilishahafanyika hii tena kipindi cha nyuma huko kujikata mara mbili kama sikosea!
 
Serikali ya DRC imeshindwa kudhibiti nchi yote kwa muda mrefu, nchi imekuwa kama pori la wezi na wanyang'anyi, hakuna utawala wa sheria. Kuigawa hiyo nchi inaweza kusaidia kiasi kikubwa kuituliza.
 
Ipo siku marekani ataanzisha choko choko hapa Tanzania na nchi itajigawa makundi kisha vita itaanza na atachagua kundi lolote na kuli brand magaidi haijalishi lipo kwenye usawa ama la, ila kwa wanaoangalia BBC news wao gaidi ni yule aliyetangazwa
 
Makundi ya Kigaidi huwezi kuyamaliza kama hujadhoofisha nguvu ya mfadhili wao

Wengi tumeona vita vya Israel na makundi yaliyokuwa yakiisumbua nchi hiyo

IDF hakuwa akipiga wanamgambo tu wa makundi ya kigaidi, bali aliwapiga na wafadhili wao wakuu na kuwadhoofisha kabisa, pale alipopiga mitambo mingi ya kutengeneza siraha na hata mitambo ya kutengeneza mabomu, rada mbalimbali za kiulinzi kule Iran na Iran akaogopa na kukaa kimya

Nchi hizi zilizoungana kupambania Congo na kupigana na wanamgambo wa M23, kwa nini sasa zisitumie mbinu hii kushambulia moja kwa moja mfadhili wa kundi hilo?

Siku hizi wapiganaji hununuliwa kwa fedha, huwezi kulishinda kundi linalofadhiliwa na nchi ambayo iko na malengo katika hilo,

Ili kushinda makundi kama hayo, ni kumpiga mfahili wao

Na ama hakuna mpango huo, basi tuendelee kupokea maiti za watu wetu kizembe

Na itafika hatua hatutakubali kupelekwa wanajeshi wetu kwenye jambo ambalo halitupi faida kama nchi zetu,

Nazungumzia hasara kwa sababu tumeamua kuukwepa kuukata mziizi wa fitina

Apigwe mfadhili wa kundi la M23 na hakutakuwa na vita tena Congo

Mungu Ibariki Tanzania, na Mungu ibariki Africa
Tuna deni la Trn 100 ambalo litalipwa na zaidi ya vizazi vyetu 10 vijavyo.

Tukijiingiza kichwa kichwa kwenye vita na M23 na Rwanda deni litapaa hadi quadrillion 10.

Idadi ya vifo vya raia( njaa, vita) itafika 10m

Bado tu unataka tuwasambaratishe M23 na Rwanda?
PS
Israeli ni taifa kubwa lina vifaa na uwezo wa kifedha kununua silaha popote. Isitoshe lina support ya EU na US.
.
 
Back
Top Bottom