Nchi zilizoendelea kama za Ulaya, Marekani na China huwa zinaongeza mishahara ya watumishi wa umma kila mwaka?

Nchi zilizoendelea kama za Ulaya, Marekani na China huwa zinaongeza mishahara ya watumishi wa umma kila mwaka?

Nchi masikini zenye uchumi unaoyumba (unstable economy) na mfumuko mkubwa wa bei (high inflation rate), hulazimika kila mwaka kuongeza mishahara ya watumishi wake ili kujaribu kukabiliana na mfumuko wa bei. Ongezeko hilo la mishahara kwa kawaida huwa ni kiduchu lakini matokeo yake huwa ni kusababisha ongezeko zaidi ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu. Yaani ni vicious circle.

Kipindi cha miaka 5 iliyopita tumeshuhudia mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu kuteremka sana na ku stabilize. Uko chini ya asilimia 3! Hivyo thamani ya hela yetu ilivyokuwa mwaka 2015 iko pale pale hadi sasa. Kwa mfano bidhaa nyingi muhimu zilizokuwa zinauzwa shs elfu kumi mwaka 2015 mpaka sasa inauzwa kwa bei hiyo hiyo au chini ya hiyo.

Siyo kweli kwamba promotions na annual increments za watumishi wa umma waliokizi sifa hawakupewa promotions na annual increments hizo ispokuwa kwa kwenye kipindi hicho kifupi cha uhakiki wa watumishi hewa na watumishi feki. Katika kipindi hiki cha miaka 5 zaidi ya watumishi zaidi ya laki tatu (ie zaidi ya 50% ya watumishi wote) walipata promotions zao baada ya kukidhi masharti yake. PAYE yao imepunguzwa nk. Kodi za kupanga nyumba nk hazipandi kila mwaka kama ilivyokuwa huko nyuma, badala yake zimepungua. Watumishi wa umma sasa hivi ni highly paid ukilinganisha na wengi walio kwenye private sector.

Huko tulikotoka private sector ndiyo ilikuwa inalipa zaidi. Ndiyo maana utumishi wa umma umetulia, hakuna migomo migomo tena kama tunazoziona kwenye nchi za majirani kwetu. Na serikali imeahidi kuendelea kuboresha mishahara yao kuendana na ukuaji wa uchumi wa nchi bila kusababisha mfumuko wa bei. Ndivyo zilivyofanya na zinavyofanya nchi zilizoendelea kama ulaya, marekani na uchina. Mambo haya ni ya kitaalamu. Si ya kimuhemuko wa kisiasa.
Huu ndio ukweli lakini watapinga...
 
Mwaka 2015 korosho kilo moja tuliuza kwa shs 3500-4000 na mwaka huu tumeuza kwa shs 2100-2200.

Mfuko wa Sulphur kwa ajili ya kupulizia mikorosho mwaka 2015 tulinunua shs 25000 na mwaka huu 2020 tumenunua kwa shs 35000-40000.

Hata gharama za ada katika shule mbalimbali za binafsi zimeongezeka kwa zaidi ya 50% ukilinganisha na mwaka 2015 lakini mishahara yetu watumishi wa serikali imebaki kuwa Ile Ile.

Siku nyingine kabla hujapost fanya utafiti kidogo usisukumwe na ushabiki wee bado kijana ukizeeka na tabia hii utakuwa mchawi.
 
Back
Top Bottom