Nawaza tu hawa walioendelea sababu kubwa ni soko lao zuri kutoka Africa. Waafrica ndiyo wateja wakubwa wa bidhaa nyingi kutoka mataifa yaliyoendelea.
Hivyo kuendelea kutusaidia siyo option ila ni kuendelea kulinda masoko yao wenyewe, maana Waafrica wakifa ambao ni wateja wao na wao wataathirika na biashara zao.
So wazungu na akina Jack Ma wataendelea kutusaidia tu wala tusihofu. Wanapata kwetu zaidi ya wanachotoa. Tuache kuwa wanyonge. Halafu sidhani kama hata wanaweza kutuletea msaada wa vifaa feki vya kupambana na covid 19 sababu huwezi ua wateja wako.
Ila tusipoungana tukawa na sauti moja itakula kwetu.maana nchi moja moja haiwezi kuwa na influence, lazima kama africa tuwe tunaongea Lugha moja.
Huwa mioyo yao inadunda pale wanaposikia kutakuwa na mkutano wa SADC au AU, EAC Summit. Ingekuwa wana uwezo wangeziulia mbali hizi organisations.