Nchi zinazoendelea hasa Afrika kwa wakati huu tuliopo hakuna ukosefu wa nafasi za kazi (ajira) tatizo lililopo ni serikali hazina pesa ya kuajiri

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
208
Reaction score
91
Kwa hali ilivyo hasa katika sekta ya elimu, afya, ulinzi na TEHAMA kuna uhaba mkubwa sana wa mtumishi.

Kwa nchi za Afrika hauwezi kusema kuna ukosefu wa ajira, hapana, changamoto iliyopo ni serikali hazina pesa ya kutosha kuajiri, baadhi ya sekta hasa nilizoorodhesa hapo juu kuna uhitaji mkubwa sana wa watumishi lakini kwa sasa inaonekana kama vile watumishi wapo wa kutosha kukidhi mahitaji kiasi cha serikali kushindwa kuajiri, lakini ukweli ni kwamba kati ya watumishi waliajiriwa katika sekta hizo pengine haifikii hata nusu ya mahitaji sahihi.

Nashauri serikali hasa za mataifa ya Afrika zifikilie namna sahihi na bora ya kushughulika na tatizo hili.
 
Sasa serikali inaweza kuajiri graduates wote?
ni kama graduactes wanakuwa wengi kuliko kawaida mahitaji ya nchi husika

wengi usoma kwa mazoea bila kujua jamii inahitaji nini mtu anasoma kile anachotaka kuwa
 
Sasa serikali inaweza kuajiri graduates wote?
Hujamuelewa OP
Sio kwamba serikali iajiri wahitimu wote. Aanachomaanisha ni kwamba, katka nchi zinazoendelea kama TZ, bado kuna uhaba mkubwa sana wa watumishi, serikali ingeweza kutatua uhaba huu, ingepunguza kwa zaidi ya 70% tatizo la ajira nchini
 
Tatizo sio serikali kuajili Bali serikali zimeshindwa kutumia rasilimali zilizopo kutengeneza ajira.
Bado bara la Afrika limekubali kutumia Kama chanzo cha malighafi na kugeuzwa masoko ya bidhaa toka nje.
Wakati nchi za Asia zinazalisha malighafi na kuuza nje huku Afrika umekuwa tofauti.
 
Kwa hali ilivyo hasa katika sekta ya elimu, afya, ulinzi na TEHAMA kuna uhaba mkubwa sana wa mtumishi.

Kwa nchi za Afrika hauwezi kusema kuna ukosefu wa ajira, hapana, changamoto iliyopo ni serikali hazina pesa ya kutosha kuajiri, baadhi ya sekta hasa nilizoorodhesa hapo juu kuna uhitaji mkubwa sana wa watumishi lakini kwa sasa inaonekana kama vile watumishi wapo wa kutosha kukidhi mahitaji kiasi cha serikali kushindwa kuajiri, lakini ukweli ni kwamba kati ya watumishi waliajiriwa katika sekta hizo pengine haifikii hata nusu ya mahitaji sahihi.

Nashauri serikali hasa za mataifa ya Afrika zifikilie namna sahihi na bora ya kushughulika na tatizo hili.
Ni sahihi, kwenye nadharia ya Uchumi Developing nations mara zote Zina iddle resources na labor shortage ila tatizo ni limited resources za kuwalipa.

Mfano hapa Tanzania hakuna sekta ambayo Haina upungufu wa staff na huo upungufu uko kati ya 40-70% ya mahitaji.
 
Back
Top Bottom