Ivi jamani ni kweli hizi mambo zinazoendelea huko mitandaoni?
Maana nimekutana na nukuu tatu tofauti kuhusu Rais Samia na Dkt Nchimbi ,je kuna ukweli wowote?
Maana nimekutana na nukuu tatu tofauti kuhusu Rais Samia na Dkt Nchimbi ,je kuna ukweli wowote?
- Tunachokijua
- Samia Suluhu Hassan ni mwanasiasa wa Tanzania na Rais wa sita wa Tanzania, anayehudumu tangu tarehe 19 Machi 2021. Yeye ni mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo na awali alihudumu kama Makamu wa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2021, ambapo alipanda na kuwa Rais kufuatia kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.
Emmanuel John Nchimbi ni mwanadiplomasia na mwanasiasa wa Tanzania ambaye kwa sasa anahudumu kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Awali alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kati ya mwaka 2012 na 2013 na kama Mbunge wa jimbo la Songea Mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.
Madai
Kumekuwepo na picha zinazosambaa mtandaoni zikiwa zimeambatana na nukuu “chadema haina uongozi wenye utimamu”,”msipumbazwe na Nchimbi mimi ndie mkuu” zikidaiwa kuwa nukuu hizo zimetolewa na Rais Samia na nukuu “bila katiba mpya nitamwaga siri zote za Samia” ikidaiwa metolewa na Dkt.Nchimbi mwaka huu.
Uhalisia
Baada ya ufatiliaji wa kurasa mbalimbali za kijamii imebainaka kuwa nukuu hizo si za kweli, kulingana na picha ya Rais Samia imebainika kuwa ilikuwa ni tukio la uwekwaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa skuli ya sekondari ya Amali,kuzindua mradiwa maji na kukagua maboresho ya kituo cha afya kizimkazi, katika kilele cha tamasha la kizimkazi 13 Aug,2026. Hakutoa kauli kama hiyo au inayofanana na hiyo
Aidha picha ya Dkt Nchimbi imebainika kuwa ilikuwa ni kwenye tukio akiwa anazungumza na viongozi wa CCM Katavi hakutoa kauli kama hiyo au inayofanana na hiyo na lilikuwa ni tukio la 13April,2024.
