DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dkt. Emanuel Nchimbi, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii nchini.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni, Dkt. Nchimbi alisema utafiti wa kina umeonesha kwamba Rais Samia amedhamiria kuhakikisha miundombinu ya nchi inaendelezwa kwa kushirikisha sekta binafsi.
Alibainisha kuwa katika sekta ya usafirishaji wa mabasi, serikali itashirikiana na watu binafsi wenye uwezo wa kununua na kuendesha mabasi ili kuhakikisha barabara zinakuwa na mabasi ya kutosha na wananchi wanasafiri kwa usalama na ustawi, hususan katika Jiji la Dar es Salaam na Jimbo la Kibamba.
Dkt. Nchimbi alisema tayari serikali imetenga fedha za kukarabati mabasi ya mwendokasi yaliyoharibika ili yarudi barabarani kwa ubora kama mapya, huku sekta binafsi ikitarajiwa kuingiza mabasi 177 mapya kwa lengo la kupunguza changamoto za usafiri wa mwendokasi.
Akigusia sekta ya afya, Dkt. Nchimbi alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Hospitali ya Mloganzila imekuwa miongoni mwa hospitali bora zaidi Afrika Mashariki na Kati kutokana na huduma za kiwango cha juu zinazotolewa, ikiwemo matibabu ya kiharusi (stroke) yanayovutia wagonjwa kutoka nchi jirani.
Alisema hatua hizo zinaonesha dhamira ya dhati ya serikali kuboresha huduma za afya kwa vitendo na kuimarisha ustawi wa wananchi.