"Kwenye mkutano wa hadhara unaweza kuongea matusi yako mengi, wakakupigia makofi lakini wakiondoka wanaenda kusimuliana, "Yule mwehu wetu ulimsikia leo? Yule kichaa tulidhani amekuwa kumbe bado" Ukiwa huna hoja umejaa matusi tu watanzania wanakudharau, wanakupigia makofi lakini kura wanakunyima.
"Vyama vyote vinatimiza jukumu la kidemokrasia kwenda kwenye uchaguzi lakini ni hiyari ya mtanzania kuamua chama kipi ameridhika nacho kumuwakilisha vizuri."
Nchimbi ameyasema hayo wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi serikali za mitaa, Mbagala, Dar.