LGE2024 Nchimbi: Ukiongea matusi wanaenda kusimuliana "Yule mwehu wetu ulimsikia leo". Wanakupigia makofi lakini kura wanakunyima

LGE2024 Nchimbi: Ukiongea matusi wanaenda kusimuliana "Yule mwehu wetu ulimsikia leo". Wanakupigia makofi lakini kura wanakunyima

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Siku ya leo wakati wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM amegusia kuhusiana tabia ya baadhi ya wagombea kutumia matusi kuwasilisha hoja akimuita mgombea huyo Mwehu na Kichaa!
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Unafikiri alikuwa akimlenga nani?



"Kwenye mkutano wa hadhara unaweza kuongea matusi yako mengi, wakakupigia makofi lakini wakiondoka wanaenda kusimuliana, "Yule mwehu wetu ulimsikia leo? Yule kichaa tulidhani amekuwa kumbe bado" Ukiwa huna hoja umejaa matusi tu watanzania wanakudharau, wanakupigia makofi lakini kura wanakunyima.

"Vyama vyote vinatimiza jukumu la kidemokrasia kwenda kwenye uchaguzi lakini ni hiyari ya mtanzania kuamua chama kipi ameridhika nacho kumuwakilisha vizuri."

Nchimbi ameyasema hayo wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi serikali za mitaa, Mbagala, Dar.
 
Back
Top Bottom