Ndairagije wewe ni genuius Tanzania haijawahi kucheza mpira Na giants yeyote yule kwa kujiamini tena ugenini

Mbegu Jr

Senior Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
152
Reaction score
178
Form is a temporal class is permanent. Mpira wanaocheza timu ya taifa kipindi hiki ni mzuri sana mapungufu ni kidogo tu tulikuwa tunalaumu washambuliaji kuto kufunga lakin jana tatizo limeonekana viungo ndio tatizo la taifa letu Back line ya timu umeijenga vizuri sana kwa kuwaweka nondo na nyoni. Nyoni alimtuma kazi nondo na nondo akaitekeleza kwa umakini mkubwa

Pongezi kwa kipa alijitahidi kuzuia vizuri ila endelea kumpa material's ya kutosha footwork yake haijawa vizuri kwenye kuanzisha mashambulio na pia timing yake inachelewa kidogo,hayo mambo akiwa klabuni kwake hayafanyiki kwa asilimia kubwa kama mpira halisi wa kisasa unavyotaka

Nimegunduwa viungo wetu wengi wanapenda kukaba kuliko kushambulia ukimtoa Farid Musa wengine wanapenda kupooza mpira wakisha pokea yaani wanalelax ndio maana mipira haiwafikii vya kutosha forwardline

But we are on right track

Akija libya hapa lazma akae tukienda kule equatorial guinea point ni za kwetu waziwazi tunisia naipa 50/50 kwakuwa hawa wenzetu wako miles nyingi mbele yetu,imani yetu tutawafunga kwa mkapa

Timu yako inacheza kwa viwango vinavyo eleweka wewe ni kocha unaetakiwa kuwepo hapo kwa kipindi kirefu kuliko kocha yeyote yule kwa maana taifa linakuhitaji kwa wakati huu muhimu wa kujenga brand ya hii nchi

Wewe ni mbegu iliyo bora kabisa
 
Nilitaka kuandika uzi kuipongeza taifa stars lkn nikasita sbb ya watu walivyoiongelea vibaya stars. Kwangu mimi jana stars walicheza mpira tena kwa kujiamini lkn kwa kumueshimu mpinzani wake. Tunisia katuacha mbali ila jana tumemkabili vilivyo vinginevyo tungefungwa nyingi wote tunalijua hilo.
 
Mwanzo mwisho nimeona mpira usiokuwa na mashabiki.wakija kwetu lazima tuwafunge sababu mashabiki watazomea na kuwachanganya TUNIS.
Nafikiri kukosekana kwa mashabiki kumetubeba hatukuwa na presha
 
Tatzo la ndairagije timu haifungi wala kutengeniza nafasi
Yuke nado afadhali ya mhilu mara kumi
Huna miksoni wala kisinda kwenye timu yako lakini vipi kuhusu dilunga
Huna chama wala tigere kweye timu yako lakini vipi kuhusu ajibu
Hata kama hapati nafasi katika timu yake yeye anawahitaji kama vile akivyokuwa hapati nafasi bale kule madrid lakini wales alihitajika
Kama vile alivyo mchezaji wa ziada giroud pale chelsea lakini ni mchezaji muhimu pale france
 
Kocha ni mzuri ila naona kama vile hujagundua tatizo la msingi la wachezaji wetu. Tatizo kubwa la timu au wachezaji wetu kwa kuangalia mechi ya jana na nyingine za nyuma ni :

1. Hawana msingi mzuri wa kucheza mpira ambao ni umiliki wa mpira ambayo ndio hatua ya kwanza kabisa katika kujifunza soka, pili hawana stamina ili ni tatizo la Taifa kutokana na umaskini wa nchi yetu mara zoote wachezaji mpira ni wale vijana walipitia maisha ya taabu (mlo taabu-chips kavu kwa wingi) ndio maana umeona jana mtu akiguswa anadondoka kama kuku.

Na mwisho ni swala kufundishwa soka kwamba soka huchezwa kwa malengo , wachezaji wetu hawaelewi hili kabisa (viungo wetu akipewa pasi hawezi kuitoa bila kujipiga chenga kwanza ahaa) inawezekana tatizo likawa ni walimu wetu pia(Hivi unaweza ukampaje Julio timu ya TAIFA ya vijana under 20?)
 
Kwa mashudu haya bila shaka wewe ni shabiki lia lia wa Mikia
 
Sitaki nikupinge, ila kwangu tunisia hana u'giant mkubwa katika wale waarabu hatari i.e Egypt, Morocco na Algeria.

Ukiangalia vizuri sisi tulikuwa na matatizo mengi, hata marking yetu ni mbovu, ni vile wao tu walishindwa kufanya maajabu au si wazuri, kuna mipira km mi3 hv miwili kapombe, mmoja kwa tshabalala, walikuwa hawako kwenye nafas zao kabisa wameacha adui, ni suala la mwenye mpira kumpasia mwenzie alete madhara golini, wakawa wanacheza utoto.

2. Viungo wetu wana matatizo, kwanza hawawezi kucheza mpira wa kuvamiwa, wako slow kiuchezaji na kimamuzi.. Kipinfi cha kwanza tunisia walikuwa wanavamia kama nyuki, walikuwa wanajichukulia mpira mingi kizeembe mnoo, yaani tunashindwa kufungua chumba na kuapsiana kwa haraka, ukiangalia jinsi walivyokuwa wanafatana viungo wetu ni km walikuwa wanakabana wenyewe, kwenye mpira usipofungua chumba, ujue ushamkaba mwenzio
Halafu mkude(labda mpira uligoma) ile style yake ya kufikiria kutoa pasi wakati mpira upo mguuni alipoteza kama mipira mi3 hivi, alikuwa ana mpira mguuni kisha anafikiria sana(anaonesha anapopiga pasi, halafu hapigi kwa haraka) wana wanaziba njia akipiga pasi.. Wenzetu wajanja katika hilj waliwawin viungo wetu.

Striker.. Sitaki kumsema bocco kushindwa kufunga, sababu hakupewa pasi ya goli zaidi ya ile dk za mwanzoni alipigiwa mpira mrefu kidogo akachelewa kipa akaucheza(angeuwahi lilikuwa goli la wazi) kuna game striker anatakiwa atumie nafasi 1 kwa gol 1, boko ni mfungaji wa goli 1 ktk nafasi 5 huko mpaka 6 tunamuona akiwa pale msimbazi.
Lakini si kila muda striker apewe pasi ya goli, anaweza yeye kujitengenezea yeye(solo goals) Ama kuwatengenezea wengine, lakini yote 9, 10 braza boko kontroo tabu.. Ktika game kama hizi boko haihitajiki, boko anahitajika kwenye zile game, wapinzani mnawaweza nyie ndio mnamiliki mpira muda wote na kutengeneza nafasi nyingi za goli ambapo boko anaweza kufunga chache.

Golikipa alicheza vizuri saana, ukitoa ile penati ambayo hatupaswi kumlaumu saana. Ni yeye pekee na mzee nyoni ndio walikuwa safi...
Yule himid mao kwa kweli simuelewi, aidha kocha anamtumia vibaya au ndio kila mmoja na bahati yake. Jamaa anakaba, kucheza shida, huyu anahitajika akicheza kiungo mkabaji, apate CM, na CAM wazuri kweli kweli. Yeye kazi yake kukaba tu, kutibua mipango ya wapinzani
 
Tumetofautiana Macho na uelewa kuitazama team imechezaje unaweza kupata presha kwa kusikiliza watu
Kwa jicho la kishabiki na pale tumepoteza tumefail watu wa kundi hili wengi ndio hata stars ikitoka hata sare na German watakuambia kocha hafai mara nyingi wanaendesha na hisia zaidi kuliko weledi
Lakini kwa jicho la ufundi pale tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwanza kwa kumuheshim mpinzani pamoja na team work ilijitahidi
 
Kwa hapa umejikita katika tatizo la kwa tuliowapa dhamana kuendeleza na kusimamia mpira
 
Huwa mnanichekesha sana mnapoendelea kusema tupo kwenye right track[emoji16] hii kauli ni ya miaka mingi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…