Unapoiongelea Ndanda si kila eneo ni la shule, ieleweke kuwa pale kuna eneo lilipo chini ya utawala wa Hospital, Kanisa na shule.
Kwa eneo lilipo Chini ya utawala wa shule si kubwa kiasi cha kuweza ku-provide eneo la kujengea msikiti, hata kanisa lilipo pale lipo chini ya eneo la kanisa, labda kama wataomba wjenge juu ya ule mlima kule nyuma ya yale ma-bweni.
Pili si kazi ya shule kutoa eneo la kujengea nyumba za Ibada. Ni jukumu la wanafunzi waamini kutafuta wapi wanaweza wakajumuika na waamini wenzao tofauti ya hapo inabidi watume maombi kwa uongozi wa shule ili uangalie namna ya kuwasaidia, ikiwepo kuwapatia majengo wanayoweza wakayatumia , ieleweke kuwa si lazima hivyo hawana haki yai kushinikiza.
Tatu ieleweke kuwa Ndanda ilikuwa ni shule ya kanisa, hivyo kama wanakuta kuna kanisa inabidi waelewe tu, na si kuishinikiza serikali kuwajengea msikiti kwani hata kanisa halikujengwa na serikali.
Moja ya matunda mazuri ambayo jamii inayategemea kutoka kwa wale walio washika dini ni busara na uwezo wa kufikiri ili kuyakabili mazingira yanayotuzunguka, kwa wanayoyafanya hawa vijana ni kujidhihirisha kuwa wao si waumini bali mashabiki wa dini.
Pia dini haijawasaidia kitu mpaka sasa kwa kushindwa kuyaelewa mafundisho yake, na badala yake mafundisho na imani vimegeuka sumu ya bonyo na nyoyo zao.