SOMENI KANUNI HIZI HAPA HALAFU MJIULIZE
.........
Uwanja wowote utakaotumika kwa michezo ya
Ligi Kuu ni lazima uthibitishwe na TFF. Kilabu
itachagua na kutambulisha uwanja wake wa
nyumbani na kuiarifu TFF/TPLB katika kipindi
cha Uthibitisho wa ushiriki Ligi Kuu.
(2) Katika mazingira maalum timu inaweza
kucheza mchezo wake wa nyumbani katika
uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na
za msingi, utambulisho wa uwanja katika
mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika
kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa
maombi maalum kwa TPLB angalau siku saba (7)
kabla ya tarehe ya mchezo husika.
(3) Katika kutambulisha uwanja wake wa
nyumbani timu itawajibika kuainisha vipimo vya
uwanja huo, aina ya majani (asili au bandia),
kama unaweza kuchezewa mechi usiku au la,
una uwezo wa kuingiza watu wangapi (stadium
capacity) na mamlaka inayomiliki uwanja huo.
(4) Endapo timu yoyote haina uwanja wa
nyumbani unaofaa kwa mchezo wa Ligi Kuu
inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au
mkoa jirani na mkoa wa timu husika ndani ya
Tanzania Bara ilimuradi uwanja huo uwe na sifa
zinazokubalika na uthibitishwe au kuidhinishwa
na TFF, baada ya uteuzi wa uwanja timu
haitaruhusiwa kubadilisha uwanja huo kinyume na
sababu za kikanuni.
(5) Kutokana na sababu za kiusalama, uwanja
kutofikika au sababu nyingine yoyote ya msingi,
TFF kwa kushauriana na timu mwenyeji husika
inaweza kuhamishia mchezo husika katika
uwanja wa mji au mkoa jirani unaokidhi haja hiyo.
(6) TFF ina mamlaka ya mwisho ya kuhamisha
mchezo katika uwanja mwingine au kubadilisha
kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa
kwa mchezo na wakati husika.
........ ......