Ndani ya Daladala!......

Ndani ya Daladala!......

Enzi zile stendi ipo mwenge,Konda kamkoromea jamaa fulani yupo simple tuu.jamaa kila akiuchuna konda anachonga tuu,nikaona jamaa kashika simu kwa muda halafu kaweka mfukoni tunakaribia kituo cha jeshi pale mbele lugalo nikaona wala wenye kofia nyekundu wapo wa3 wanaelekeza gari ielekeee kule ndani.........Itaendelea.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Unakuta gari liko moja na lishajaa ila konda anazidi kusema sogea nyuma" Abiria unaanza kuhamasisha tushuke wote tuu"konda anakuchora tuu,ile unashuka tu anagonga gari iondoke.....
 
Siku moja nilishuhudia konda kagoma kumpakia abiria fulani maeneo fulani baada ya gari aliyopanda kuishia njiani kisa eti Yule abiria aliringa kupanda gari yake kule kituoni sasa kamkuta tena mbele anamwambia we si una haraka!
 
napenda sana daladala siku moja moja hua napanda hasa mwendokasi nikiwa dar. ila mwendo wa huku zanzibar ni tofauti
 
Hakuna kinacho niuzi kama mishuzi!
 
Kweli tupo wachache ila hata wale wanaotumia magari kuanzia tarehe 1 mpaka 10 alafu baadae wanazimikiwa mafuta mwisho wa siku kuanzia tarehe 20 wanamalizia mwezi kwa kupanda daladala si wenzetu pia.

Back to the topic: mara daladala linapishana na gari ndogo bahati mbaya mwenye gari ni mwanamama sasa namna ya kuachiana njia inakuwa shida "amehongwa gari huyo dada siku mbili tu ameingia barabarani, anatuchelewesha" na akiwa mwanamume..."gari lenyewe la mkopo alafu anatuwekea usiku hapa"
[emoji23] [emoji23] gari lenyewe la mkopo hii hua naitamka sana hii
 
Juzi kati nimepanda UDART. Bas kulikuwa mshua mmoja anakanyaga popote pale iwe ni juu ya mtu au juu ya mguu wa mtu, kwake sawa tu. Ikabidi nisimamie mguu mmoja halafu mguu mwingine unashuka kwa machale pale napopata upenyo.
Watu kama hao inabidi umkanyage yeye makusudi
 
Back
Top Bottom