Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Kinadharia upo sahihi uyasemayo ila kiuhalisia ni tofauti sana.Nadhani mmoja ya kazi za Tume ya Uchaguzi na vyama vya siasa ni kuwapa wananchi elimu ya upigaji kura. Ni bahati mbaya kwamba vyama vya siasa vinajikita kwenye kulumbana badala ya kuwaonesha wananchi / wapiga kura ni kwa nini wao wanafikiri wakiwa madarakani watakidhi matarajio ya wananchi ili kwayo wananchi waamue ni nani wampe kura.
Aidha baadhi ya viongozi kuhama vyama vyao kunaashiria kwamba hata wao ama hawajui wafanyacho au wanajua walifanya makosa kuingia huko wanakotoka.
Kimsingi tukubaliane kwamba: "Katiba nzuri inatoa Tume ya Uchaguzi nzuri na Tume ya Uchaguzi nzuri inatoa viongozi wazuri (baada ya wananchi kuelemishwa vizuri juu ya namna nzuri ya kuchagua viongozi wao) na viongozi wazuri (kutokana na vyama kuwa makini juu ya kuteua wapigiwa kura) watatoa matokeo mazuri ambayo yataipeleka mbele nchi yetu kwa uzuri"
Bado nasimamia hoja yangu kwamba "raisi aendelee kuchaguliwa kwa kura, na sio kwa mihula"!
Elimu ya upigaji kura ya miezi isiyozidi 6 au tuseme mwaka 1 haiwezi kuwa mbadala wa elimu ya sekondari na ya elimu ya juu.
Elimu ya upigaji kura haifundishi kuongeza uwezo wa kufikiri namaanisha haiongezi reasoning capacity ya mtu kwa kiwango kama cha elimu ya sekondari na kuendelea elimu ya juu.
Katika hali yetu ya umasikini bado rushwa ktk uchaguzi ni kikwazo hata mbele ya elimu ya upigaji kura.