Uda pole mwaya.
Kwanza unatakiwa ujue kwamba haiwezekani kabisa kumbadilisha mtu ambae yeye mwenyewe HATAKI kubadilika. Utapiga kelele sana, utalalamika sana, utalia sana ila hamna kitakachobadilika zaidi ya kumfanya aone unamchosha na matakwa yako ambayo sio yake.
Swala la kuvuta sigara kwa mfano. . . unaweza ukajitahidi kumwambia kuhusu madhara yake katika hali ya utulivu badala ya kumwambia tu "mi sitaki uvute sigara" na kuwa kama unampangia maisha. Mweleze kiasi gani harufu yake inakuboa anapokua karibu na vitu kama hivyo.
Pombe kwakweli kumtaka mtu ambae amezoea kunywa aache tu ndani ya siku au wiki ni kama unamuonea. Kama unywaji wake sio ule uliopitiliza, yani hanywi mpaka akirudi anapepesuka na kuanguka hovyo, hawi mgomvi basi acha afurahie bia zake mbili tatu. Jua kadiri utakavyoendelea kulalamika na kumuagiza aache ndio unamsukuma aongeze hata muda wa kukaa huko Bar kwasababu anajua akirudi kwako ni kelele. . kelele.
Na kama ni muhimu sana kwako yeye kuacha hayo mambo na yeye haonyeshi utayari wa kufanya hivyo fikiria kuhusu kuvunja hayo mahusiano. Nakwambia hivi kwasababu kama anakukera sasa hivi usitegemee atabadilika mkiona kwasababu hamna uhakika wa hilo. Hivyo either umkubali kama alivyo mapema hii ili isikusumbue baadae ama uangalie kwingine. . .