Ndani ya miaka 10, uchumi wa Tanzania utaimarika sana kutokana na uwepo wa graphite, nickel, rare earth elements, helium, uranium, dhahabu na CNG

Ndani ya miaka 10, uchumi wa Tanzania utaimarika sana kutokana na uwepo wa graphite, nickel, rare earth elements, helium, uranium, dhahabu na CNG

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
CHADEMA nataka niwape sababu mojawapo kwa nini CCM katika kipindi hiki hawatakubali kwa njia yeyote kuachia madaraka.

CCM wanajua sana kwamba ndani ya miaka 10 ijayo, uchumi wa Tanzania unaweza kufikia kiwango cha nchi kama Afrika Kusini na kina Misri. Na hili linatokana na kwamba ndani ya kipindi hicho tutakuwa tunapata fedha nyingi za kigeni kutokana na exports za graphite, nickel, rare earth elements, helium, uranium, gold, almasi na huenda hata mafuta. Utalii wa mbuga za wanyama utaendelea kuwa na mchango wake pia.

Kwa sasa Tanzania inafikiria kuanza kujenga mitambo ya kutengeneza diesel na mafuta ya ndege kwa kutumia gesi tuliyo nayo. Hatutatumia fedha ya kigeni kuagiza haya mafuta.

Yote haya yanaonyesha kwamba katika miaka kumi ijayo, Tanzania haitashindana tena na kina Kenya na Uganda kwenye uchumi na maendeleo, bali tutakuwa tunacheza ligi na Afrika Kusini, Egypt, Morocco, Nigeria nk

Sasa CCM wanajua hili, na hawako tayari kuona kipindi hiki cha neema kije wakati wao ndio chama cha upinzani ili ionekane Chadema ndio walioleta neema kwa Tanzania.

Madini haya yatasababisha serikali kuwa na fedha za kutosha kuboresha barabara zote kuu na ndogo kwa kiwango cha lami, reli, huduma za maji, umeme, huduma za afya, elimu, usafiri na huduma nyingi nyingine za jamii. Tutaweza kupeleka SGR hata huko Mtwara, Arusha na Musoma, kwa fedha zetu wenyewe.

Serikali haitategemea tena kodi za wananchi, na vitu kama miamala ya simu itakoma, na bei ya umeme, nauli nk zitashuka sana na kila mtu ataipenda serikali na chama kitakachokuwa madarakani.

Sasa CCM wakijua hili, ni kwamba hawatakubali kuondoka madarakani hata kwa njia gani. Ikibidi kuteka, kuua, kutumia polisi, kutumia TISS, kutumia JWTZ nk, watafanya hiyo ili wao waje kuwa chama tawala wakati wa hizi neema.

Dhuluma zinazofanywa na CCM kwa sasa ni katika hii strategic thinking. Mkijua hili basi mnajua what is at stake, na jinsi ya kukabiliana na hali halisi.

Sikilizeni msikie.
 
Kinachoweza kuzuia hayo maendeleo ni kuendelea kuwa na ufisadi wa kiwango cha viongozi waliopo sasa madarakani
 
Halafu kuna watu wanaleta vurugu zao watu wasile matunda ya uhuru kwa amani.

Chadema ni mashetani.
 
Halafu kuna watu wanaleta vurugu zao watu wasile matunda ya uhuru kwa amani.

Chadema ni mashetani.
Labda ni kweli Chadema ni mashetani, lakini CCM ni walafi na wauaji, hilo liko wazi
 
Kuna nchi ukiongozi wake mkuu aliwahi nukuliwa akisema
"Mimi ndiye kiongozi mkuu Wa nchi wa mwisho kuongoza nchi hii ikiwa masikini"

Sababu ya kauli hiyo ilikuwa uwekezaji katika magesi gesi.

Ajabu, mpaka sasa kiongozi mkuu Wa nchi Huwa ananukuliwa akisema sisi bado ni nchi masikini.

Hivyo mleta mada, acha kutupanga na visitori vya kijinga jinga Kila mara.

Nchi haitaondokana na umasikini kisa imegundua graphite n.k bali kwa mipango madhubuti na endelevu.
 
Kwa ufisadi na wizi wa sasa wa mali zetu, hata yangechimbwa madini mengi sana sana sana, bado tutaendelea kuwa maskini.
 
Back
Top Bottom