Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kiufundi unaweza ukasema ni mawaziri watano. Lakini pia ukisema ni mawaziri wanne napo utakuwa hujakosea maana kuna huyo mmoja alirithiwa na baadaye kidogo ndo akabadilishwa.
Ni hii wizara ya mambo ya nchi za nje.
Hivi kuna nini hapo wizarani? Katika awamu hii tokea 2021, mawaziri wake wengine hawajadumu hata mwaka mmoja kwenye hiyo nafasi.
Yule aliyetumbuliwa juzi yeye kadumu kwa miezi 10, kama sijakosea.
Na tokea 2021, hiyo wizara imeongozwa na watu wanne tofauti.
Hivyo, kwa wastani, mawaziri wa hiyo wizara kwenye huu utawala wa Samia, hawadumu zaidi ya mwaka.
Wanadumu kwa takriban miezi tisa hivi.
Tatizo ni wao au mteule wao?