Ndani ya vyama vya siasa upinzani Tanzania gumzo na hoja kuu ndani ya vikao vyao ni Samia Suluhu Hassan tu 2025

Ndani ya vyama vya siasa upinzani Tanzania gumzo na hoja kuu ndani ya vikao vyao ni Samia Suluhu Hassan tu 2025

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Wengi wao wako radhi, na wameridhia kuunga mkono jitihada za Dr. Samia Suluhu Hassan za sasa; na endapo pia ataamua kugombea ukuu wa nchi kwa ngwe nyingine ya pili, basi watamuunga mkono kwa 100%.

Kuna wanachama wachache miongoni mwa vyama hivyo vya siasa vya upinzani, wanajaribu kuweka vikwazo kwa kuimpose some demands kana kwamba jambo hili ni la Lazima.

Kama unaona jitihada za makusudi za Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo, iweje kwenye kumuunga mkono unaweka vigezo na masharti ndugu mzalelondo?

Tuwe wangwana ndugu zangu wananchi. Hebu tusimame pamoja na huyu mama, Rais wetu kipenzi Dr. Samia Suluhu Hassan kwa hiyari za dhati za mioyo yetu yetu, kwa kwa uzalendo wetu na maslahi mapana ya waTanzania wote.

Asante sana kwa uzalendo na upendo wenu wa dhati kwa Taifa, vyama ambavyo tayari vimekwisha kuamua kutokusimamisha mgombea urais uchaguzi ujao, badala yake kuungana na mamilioni ya waTanzania kote nchini kumuunga mkono kiongozi shupavu sana na mchapakazo Dr.Samia Suluhu Hassan.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwani ni lazima wote tuwe kondoo?

Acha wengine tubakie kuwa chui...
 
Nyinyi mnaobeba ajenda mama aendelee 2025 sidhani akili yenu iko sawa. Haihitaji akili nyingi kufahamu mama kuwa makamu wa Rais miaka 5 na Rais miaka 5 inatosha kabisa sabab tayari miaka 10 kama kiongozi wa nchi kikatiba inatimia, huhitaji kuongeza!

Cheo cha makamu wa Rais na Rais tofauti yake ni ndogo sana kiutendaji na hivyo bahati aliyoipata mama kuhudumu ndani ya miaka 10 kuwa makamu wa Rais na Rais inatosha kabisa kuweka mchango wake kwa nchi!

Ni nadra sana kupata nafasi km hii mama aridhie kutogombea ili apatikane mwingine, Mungu hajawahi kuumba superman na mambo ya uchaguzi yanategemea sana changamoto zilizopo kwa wakati huo na hivyo kuelekeza aina ya mtu anayeweza kukabiliana na changamoto hizo, uchaguzi si suala la mazoea au utamaduni ni maisha ya watu kuwapa urahisi na nafuu kwenye maisha yao.
 
Back
Top Bottom