Ndege 3 za Air Tanzania (Air Bus) zimepata hitilafu ya kiufundi, haziruki

Ndege 3 za Air Tanzania (Air Bus) zimepata hitilafu ya kiufundi, haziruki

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kusimama kwa ndege hizo za Shirika la Ndege (ATCL), aina ya Airbus a220-300 kumetokana na hitilafu ya kiufundi na ambapo watengenezaji waliagiza zisiruke.

Amesema Serikali inaendelea na mazungumzo na watengenezaji kuhusu matengenezo ya Ndege hizo ili zikae sawa na kuendelea na shughuli za usafirishaji.

Msigwa ameongeza kuwa tatizo hilo limezikumbuka kampuni nyingi za Ndege duniani na ni jambo la kawaida kutokea kwenye masuala ya kiufundi.

"Amesema Serikali inaendelea na mazungumzo na watengenezaji kuhusu matengenezo ya Ndege hizo ili zikae sawa na kuendelea na shughuli za usafirishaji."

yaani mpaka leo bado tuko kwenye mazungumzo na Airbus? kiasi gani tunapoteza? usumbufu kiasi gani unatokea huku ikizingatia tumemonopolize biashara kwa kumuondoa competetor.
 
Msigwa ameongeza kuwa tatizo hilo limezikumbuka kampuni nyingi za Ndege duniani na ni jambo la kawaida kutokea kwenye masuala ya kiufundi.
Kwani zilishawahi kuruka zaidi ya ile iliyotoroshewa Uholanzi?
 
Tumefika Huko Sasa Hapo Ujue Tutapigwa Sungunyo Toka Ukraine Ya Pesa Ndege
 
Msemaji wa Serikali angejikita kwenye siasa huku kwenye mambo ya Taaluma wangesema Ma Eng wa ATCL sio kuja na majibu wamesema tupaki basi kama vile ni mradi wa daladala.
 
Hii inaitwa Grounding, na ni kawaida endapo ndege moja ya aina hiyo popote duniani inapopata tatizo na wakagundua tatizo la kimfumo, mtengenezaji huagiza ndege zote duniani alizotengeneza za aina hiyo zisiruke hadi atakapozifanyia maboresho
 
Ni kweli kampuni inaweza kuagiza kwamba ndege za aina fulani zisiruke mpaka hitilafu fulani ipatiwe ufumbuzi, lakini tatizo ni huyu msemaji. Alishajijengea mazingira ya kutoaminika kwa kusema uongo mara kwa mara, hivyo watu hawawezi kuamini tena anayosema.
 
Hii inaitwa Grounding, na ni kawaida endapo ndege moja ya aina hiyo popote duniani inapopata tatizo na wakagundua tatizo la kimfumo, mtengenezaji huagiza ndege zote duniani alizotengeneza za aina hiyo zisiruke hadi atakapozifanyia maboresho
Hili ni kweli na linatokea tu mara kwa mara. Tatizo ni huyo anayetoa taarifa. Haaminiki hivyo watu wengi hawataamini japo linaweza kuwa kweli. Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa serikali kujenga trust kwa wananchi wake. Nashauri mfumo wa kutoa habari wa serikali ufumuliwe, halafu atafutwe mtu mpya aanze upya na asiwe na porojo kama huyu jamaa.
 
Ivi mnadhani hizo taarifa zinatoka kwa bahati mbaya ama kwa mtoataarifa kutokuwa na weledi??.

Kilakitu kinapangwa kuanzia juu mpaka chini mkuu siokama hawana utaalam.
 
Hii Serekali ya akina Haambiliki kweli!. Makosa yaliyofanyika kwa kununua ndege za Bombardier 300 wakati ndege hizo zinafanana na Airbus 320 ndio makosa yale yale yaliyofanyika kuagiza ndege za Boeing 737 max ambazo bado zina mgogoro!
Hivi hizi hasara zinazotengenezwa zinafidiwa namna gani? Kulikuwa na sababu gani ya kuwafurusha fastjet? 🤔
 
Back
Top Bottom