Ndege 3 za Air Tanzania (Air Bus) zimepata hitilafu ya kiufundi, haziruki

Ndege 3 za Air Tanzania (Air Bus) zimepata hitilafu ya kiufundi, haziruki

Hii inaitwa Grounding, na ni kawaida endapo ndege moja ya aina hiyo popote duniani inapopata tatizo na wakagundua tatizo la kimfumo, mtengenezaji huagiza ndege zote duniani alizotengeneza za aina hiyo zisiruke hadi atakapozifanyia maboresho
Kweli kabisa
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kusimama kwa ndege hizo za Shirika la Ndege (ATCL), aina ya Airbus a220-300 kumetokana na hitilafu ya kiufundi na ambapo watengenezaji waliagiza zisiruke...
Imeisha hiyo, maskrepa yamepaki na kuwa makazi ya popo.

Msigwa hauwezi kutudanganya midege mibovu hiyo.
 
Kama tatizo ni la muundaji tuondoe hofu bilashaka atarekebisha hitilafu na kutulipa hasara
 
Lakini nimependa hapo ambapo mtengenezaji ameagiza ndege hizo mbovu zisiruke.

Kwa mambo ya kienyeji haya mmnh!

Afadhali Mwenyezi Mungu ameepusha mbali vifo vya innocent people
 
Yaani wametuuzia ndege mbovu ili waendelee kutupiga kupitia matengenezo yake.

Hivi hakuna namna tunavyoweza kudai fidia kwa siku zote ambazo zitakuwa hazifanyi kazi?
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kusimama kwa ndege hizo za Shirika la Ndege (ATCL), aina ya Airbus a220-300 kumetokana na hitilafu ya kiufundi na ambapo watengenezaji waliagiza zisiruke.

Amesema Serikali inaendelea na mazungumzo na watengenezaji kuhusu matengenezo ya Ndege hizo ili zikae sawa na kuendelea na shughuli za usafirishaji.

Msigwa ameongeza kuwa tatizo hilo limezikumbuka kampuni nyingi za Ndege duniani na ni jambo la kawaida kutokea kwenye masuala ya kiufundi.


Tunaendesha biashara ya ndege kisiasa eeehhh!!? Tutaona!
 
Hivi hii haiwezi kufanana na mabehewa ya Sgr kweli? Tuliambiwa mapya kumbe mitumba ilikarabatiwa.

Haiwezekani ndege Kila siku ni gereji na tunaambiwa ni mpya.👇
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kusimama kwa ndege hizo za Shirika la Ndege (ATCL), aina ya Airbus a220-300 kumetokana na hitilafu ya kiufundi na ambapo watengenezaji waliagiza zisiruke.

Amesema Serikali inaendelea na mazungumzo na watengenezaji kuhusu matengenezo ya Ndege hizo ili zikae sawa na kuendelea na shughuli za usafirishaji.

Msigwa ameongeza kuwa tatizo hilo limezikumbuka kampuni nyingi za Ndege duniani na ni jambo la kawaida kutokea kwenye masuala ya kiufundi.


serikali inaagiza vitu vingi ambavyo ni mitumba kasoro magari tu,hata mabehewa ya treni yenyewe ni mitumba halafu kwa nn wanaagiza ngdege bila kuwaandaa mafundi?
 
ATCL mnaulizwa Kwanini mitandao ya kufanya malipo mnataka Vodacom peke yake?

Kwani wananchi wwnatumia Vodacom wote? [emoji57]

Mna fahamu kwamba kwa kufanya hivyo mnasababisha usumbufu mkubwa kwa watu?

Halafu Eti na Simbanking ya kampuni moja tu ?
 
Mifumo yenu ya malipo inapaswa kuwa rafiki kwa matumizi na sio vikwazo chungu nzima! [emoji57]

Kuna mtu amewa-mind kinoma!

Sio wananchi wote wanatumia Vodacom.

Wekeni mitandao walau 2-3 na sio mtandao 1 Kwanini mna Fanya monopolization?

Mbona taasisi nyingine za serikali wanaweka wigo mpana wa mitandao yote kuweza kufanya malipo?

Sijui kama mnajua usumbufu wake ulivyo mkubwa.!
 
Yaani kurudi kwenye shirika moja lisilo na ushindani ni shida kubwa sana Kwa wananchi.
 
Kwa hiyo watu walazimike kwenda mbali kutafuta line za Vodacom kwa lazima ili kufanya malipo ya nauli ya ATCL?

Safari yenyewe ukute ni ya mara moja Kwa mwaka kisha hiyo line ya Vodacom kisha ataitumia wapi ? [emoji2369]
 
Hizi ndege wanasiasa ndiyo watakuwa walizipitisha na kuzinunua
Bila kuwashirikisha wataalam wa ndege

Ova
 
Msigwa ndio msemaji wa Air Tanzania? Je Air Tanzania hawana msemajai wao hadi wawe wana tumia msemaji wa Serikali? na vipi Mashirika mengine ya Uma pia ni yeye huwa anayasemea?
 
Back
Top Bottom