Uchaguzi 2020 Ndege, barabara na flyovers vilitakiwa viwepo miaka mingi iliyopita. CCM wametuchelewesha. Tukipe nafasi chama kingine

Uchaguzi 2020 Ndege, barabara na flyovers vilitakiwa viwepo miaka mingi iliyopita. CCM wametuchelewesha. Tukipe nafasi chama kingine

Baada ya kusikiliza hotuba ya Magufuli akiwa Geita inasikitisha kuona anazidi kupotosha watu.

Anasema kwamba huu si wakati wa kufanya majaribio kwa kukichagua chama kingine, mimi napingana nae. Ki ukweli, huu ndio muda muafaka wa kukipa dhamana chama kingine. CCM ilipewa dhamana zaidi ya miaka 50 lakini wamezidi kututia umasikini. Hizo ndege, fly overs, barabara n.k. tungetakiwa tuwe navyo siku nyingi sana lakini ni CCM ndiyo iliyotuchelewesha!

Amesema pia serikali yake haiingilii dini, hili pia sio kweli. Kuna viongozi wengi wa dini wanabughudhiwa kuhusu uraia wao pale wanapoikosoa serikali. Je Magufuli anasemaje kuhusu hili?

Huu ni wakati muafaka wa kukipa nafasi chama kingine. CCM ilishapewa nafasi kwa zaidi ya nusu karne ikaichezea.


CCM inashinda kwa sababu ya Uelewa mdogo wa Watanzania wengi, siasa za udini mfano uchaguzi wa 2010 Mahakama ya kadhi,Ukabila mwaka 2015 na mwendelezo wake wa kuwatumia wasukuma kama Chambo cha kupata kura kutokana na wingi wao, vitisho vya kutumia baadhi ya wakuu wa vyombo vya dola ambavyo kimsingi ni wakubwa wachache wanaoshirikiana na watawala kukwapua mali za umma na kujilimbikizia mali hivyo wanahofia nyadhifa zao endapo chama kingine kitatawala. Hata hivyo mwamko wa watanzania kutafuta haki na usawa ni mkubwa sana.

Upendeleo na ahadi za madaraka mdio unaowafanya wakuu wa vyombo kuwa tayari kuwaua watanzania wote alimradi wapewe madaraka na CCM .
Hawa ni sawa na wale wanaotafuta utajiri kwa njia ya kutoa makafara ya wazazi wao au watoto wao.
Ndio maana wanaungwa mkono na taasisi za dini zenye kufanyaiujiza ya kitapeli na kichawi.

Amani haiji bila haki na uhuru.
Mtu akitendewa hali na kufurahia uhuru wake hawezi kuvuruga amani lakini mtu akiona Chama kimoja ndio kinajiona kuwa wao ndio waliomba hii dunia.
 
We kibaraka tu wachama huwezi nikataza kalale ukue mi ndo tayari nishachukua bendera ya chadema ila mkizingua narudi CHAUMA maana na nyinyi mnaweza amka mkasema tz kuna korona..😂😂
Corona ipo..Farid Musa mchezaji wa Yanga kanyimwa visa ya Turkey kwenda kufanya trial kisa Waturuki wameiweka Tanzania kwenye black list ya corona..Magu umeuwa ndoto ya kijana wa Kitanzania..uliambiwa fanya partial lockdown ukabisha..unajifanya unamjua Mungu kuliko Israel na Saudi Arabia walifunga mpaka kuhiji
 
Jengo tu la ofisi ya makao makuu ya CHADEMA mna miaka zaidi ya 25 hamkujenga ndio muweze kujenga nchi?

CHADEMA si chama tajiri kwahiyo hiyo hoja naitupilia kwenye pipa la taka.

Ila kitu kimoja nina uhakika nacho, CHADEMA ikipewa ridhaa na wananchi haitatumia hovyo pesa ya walipa kodi kujenga kiwanja cha ndege kijijini kwa Tundu Lissu!
 
Back
Top Bottom