Wakati mwingine hao wapinzani wana hoja!
Mtu hawezi toka kwenye nyumba ya tembe aende kupanda BOEING 878.
Tununue mandege sambamba na kuboresha maisha halisi ya mtanzania mmoja mmoja!
Nimesikia tuna mapesa mengi, huku tunawadhibiti mabeberu wanatupa pato zuri kwenye rasilimali zetu. Hivyo, tunajiweza sana.
Juzi
Mzee Mwanakijiji alikuja na hoja nzuri sana ya namna ya kupambana na kutokomeza makazi duni ya tembe na kukarabati shule zilizochoka ziwe na muonekano wa kisasa!
Haiwezekani tujisifu tuna mandege huku watoto wanavaa kaptula zenye viraka na kusoma kwenye sakafu za udongo. Vumbi, bacteria, virus, tuberculosis, pumu, na kila kitu humo!
Umasikini katika individual basis ni mkubwa sana! Hasa vijijini!