Tetesi: Ndege ingine ipo hatarini kukamatwa

Tetesi: Ndege ingine ipo hatarini kukamatwa

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kampuni ya kuzalisha umeme ya
Symbion nayo imefungua kesi ya
madai. Inaidai serikali dola milioni 561.
Ile ndege inayotaka kuanza safari za
London itakuwa hatarini kukamatiwa
huko.
Serikali ilichukua jukumu la kumiliki
ndege ili kukwepa zisikamatwe
kutokana na madeni ya ATCL huku
ikiendelea kuyapunguza taratibu.
Ila hawakuliona hili la kwamba serikali
yenyewe pia ina madeni, tena madeni
yake ni makubwa kuliko madeni ya
ATCL.
Na hawakuliona hili la kwamba nchi
zingine wanaruhusu ukamataji wa mali
za serikali kwa ajili ya kesi za madai.
Sisi nchini kwetu Tanzania hairuhusiwi
kukamata mali ya serikali kwa madai
yoyote yale.
Ni wakati sasa wa kupanga na
kuchagua.
Moja kutathmini madeni ya ATCL kama
yanaweza kulipika ili umiliki wa ndege
uhamishiwe ATCL.
Au kama madeni ya ATCL nayo bado ni
hatari basi kutengeneza kampuni mpya
ya umma (yaani PLC) ambayo itauziwa
hizi ndege izimiliki. Kampuni hiyo hisa
zake ziuzwe soko la hisa iwe ni
kampuni ya Watanzania wote. Maana
hizi ni ndege za Watanzania.
Kampuni hiyo pia ipewe misamaha ya
kodi, maana sidhani kama taasisi ya
serikali inayomiliki hizi ndege kwa sasa
inalipa kodi.
Kampuni mpya itaondoa kabisa hili
gundu la ndege kukamatwakamatwa
 
Dawa ni moja tu hizi ndege zimilikiwe na kijiji cha kolomije iishie hapo maana sizani kama kijiji cha kolomije kina madeni huko nje
 
Cku moja john akienda nchi wanakotudai wamkamate yeye wabaki nae huko huko
 
Back
Top Bottom