Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,692
Reaction score
3,891
Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki, Je wamejipanga kufika huko kiushindani?

A9D7BC34-C331-4BAB-A9CC-94064CB1C20A.jpeg
 
Mashirika makubwa ya ndege kama SAA, KQ hata Emirates na KLM yamekuwa na changamoto kubwa za kibiashara na hata kufilisika.

Angalia SAA ya Afrika Kusini inajitahidi kufufuka kwa taabu kubwa, hili ni shirika lenye ndege zaidi ya 120 na hufanya safari zake popote duniani!

Isitoshe linamilikiwa kwa ubia na wazungu na serikali tajiri ya Africa Kusini. Sijui itakuwaje na ATCL yetu kama tu tunashindwa hapa nyumbani kuendesha TTCL na TANESCO kibiashara.
 
Mashirika makubwa ya ndege kama SAA, KQ hata Emirates na KLM yamekuwa na changamoto kubwa za kibiashara na hata kufilisika. Angalia SAA ya Africa Kusini inajitahidi kufufuka kwa taabu kubwa, hili ni shirika lenye ndege zaidi ya 120 na hufanya safari zake popote duniani!, isitoshe linamilikiwa kwa ubia na wazungu na serikali tajiri ya Africa Kusini. Sijui itakuwaje na ATCL yetu kama tu tunshindwa hapa nyumbani kuendesha TTCL na TANESCO kibiashara.
Kwa hili tayari tunahesabu hasara kubwa kisa maamuzi ya mtu mmoja tu.
 
Back
Top Bottom