Serikali yetu ilikuwa nia njema sana kufufua atcl lkn kimtazamo ni km hatukujipanga sababu biashara ya ndege ina mnyonyororo mrefu sana ktk uendeshaji wake mosi shirika ni lazima liwe na mawakala wa kutosha ndani na nje ya nchi wa mauzo ya ticket pili kwa kuanzia shirika angalau lingekuwa na safari ktk miji mitano mikubwa kibiashara na utalii mfano Mumbai India.. Guaxhuu China...Johannesburg South Africa London UK na magharibi ya Africa kuna shida sana ya usafri ni Ethiopia airline peke yao ndio wanakwenda huko ktk mashirika ya kiafrika na nauli zpo juu kuliko hata ulaya..Kwa kutumia hz Dreamline na airbus shirika linaweza kuoperate hz route tena kwa faida na baadhi ndege zikawa zinatumika uber kukusanya abiria ktk nchi majilani zetu km Congo,Zambia, Burundi, Malawi, Uganda,nk kwani nchi zote hz kwa sasa hazina shirika madhubuti km atcl..Tatu shirika lilitakiwa kuingia mikataba na mahotel kwa ajili ya abiria wanakuwa transit pamoja na usafiri wa uwakika kutoka Airport kwenda mahotelini hiki kitu Ethiopia airline wamefanikiwa sana ..Nne Kupunguza ghalama za uendeshaji mashirika mengi yanakufa ama kujiendesha kwa hasara sababu kubwa ni ghalama za uendeshaji unakuta soda ya kopo supermarket inauzwa 1000 lkn mzabuni analiuzia shirika la ndege 20,000 uwo mfano mmoja kati ya mingi ndio mwisho wa siku shirika linaonekana linaendeshwa kiasara lkn ukweli kbs hasara nyingi ni zakutengeneza ..Tano na mwisho hapa ndio kwenye tatizo kubwa Africa inaonekana usafri wa ndege ni anasa na ni kwa ajili ya watu flami tu ili ni tatizo kubwa nauli one way kwenda kigoma 500,000 tsh wakati nauli ya Dubai kwa fly Dubai 370 usd go and return..jibu rahisi nauli ya Dubai rahisi kuliko kigoma kwa ndege..Hv kipi bora kuweka nauli ya 500,000 kwenda kigoma alafu unapata abiria saba au nauli ya 200,000 upate abiria arobaini ..mwisho biashara ya ndege angani sio ardhini kuna mikoa km mwanza kigoma kilimanjaro,mbeya, dodoma inatakiwa iwe hata na route kumi kwa siku km nauli itakuwa rafiki hayo ndio maoni yangu km mtanzania mpenda nchi yangu