Kumekuwepo na dai kuwa Ndege wanaweza kukaa kwenye nyaya za umeme bila kupigwa na shoti kwa sababu umeme haupitii kwenye miili yao.
- Tunachokijua
- Lakini kupitia ufuatiliaji wa njia ya mtandao ambapo chapisho la MIT School of Engineering linaeleza kuwa ndege anayekaa kwenye waya mmoja wa umeme kwa kawaida hapigwi na shoti kwa sababu miguu yake yote miwili huwa katika kiwango cha umeme kinachokaribiana.
si kwamba waya hauna umeme au kwamba mwili wa ndege hauwezi kuendesha umeme. Badala yake, tatizo kubwa ni njia ambayo mkondo wa umeme unaweza kupita. Ndege akiwa amekaa kwenye waya mmoja tu, hakuna njia muhimu ya mkondo kutoka kwenye waya huo kupitia mwili wake kwenda kwenye sehemu yenye tofauti ya kiwango cha umeme.
Sambamba na hilo kupitia chapisho la U.S. Geological Survey (USGS) linabainisha kuwa ndege hupigwa na umeme pale mwili wake unapounganisha sehemu mbili zenye umeme au sehemu yenye umeme na sehemu iliyounganishwa na ardhi.
Vilevile, ndege anaweza kupigwa na umeme akigusa waya wenye umeme na sehemu ya chuma iliyounganishwa na ardhi kwa wakati mmoja. USGS inaeleza kuwa hali hii inaweza kusababisha mkondo wa umeme kupita kupitia mwili wa ndege na kusababisha kifo.
Ndege wanaweza kukaa kwenye waya wa umeme bila kupigwa na shoti lakini si kwa sababu umeme haupo kwenye waya. Ndege huwa salama zaidi anapogusa waya mmoja pekee kwa sababu hakuna tofauti kubwa ya kiwango cha umeme kati ya miguu yake inayosababisha mkondo kupita kwenye mwili wake.
Sambamba na hivyo kumekuwepo na jitahada kadhaa zinazofanywa na baadhi ya mashirika ya umeme duniani ikiwepo kuongeza nafasi kati ya nyaya za umeme pamoja na kuweka vifuniko maalum vya kinga kwenye nguzo za usambazaji wa umeme.
Mikakati hiyo inalenga kupunguza uwezekano wa ndege, hasa wenye mabawa mapana, kugusa nyaya mbili kwa wakati mmoja au kugusa waya wenye umeme pamoja na sehemu ya chuma iliyounganishwa na ardhi, hali ambayo inaweza kusababisha kupigwa na umeme au kufa.