Ndege ya Air Tanzania iliyotokea KIA kupitia Zanzibar asubuhi tarehe 7/12/2023 tairi la nyuma limekwisha, libadilishwe!

Ndege ya Air Tanzania iliyotokea KIA kupitia Zanzibar asubuhi tarehe 7/12/2023 tairi la nyuma limekwisha, libadilishwe!

Kwahiyo watu wakae kimya wakiona tatizo, kisha yakitokea maafa mtoke nyie mliochagua kukaa kimya kusema hayo ni mapenzi ya Mungu?!
Watafupisha ziara huko ughaibuni na kurudi Dodoma kisha wanakaa siku 4 ndio wanaenda kwenye eneo la ajali kisha wanaitwa wazalendo "mitano tena"!
Bangladeshi!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Usikute rubani alishatoa taarifa muda mrefu kuwa muda wa tairi kuruka na kutua umeisha, akajibiwa bajeti yake haijatengwa asubiri kidogo wataiandikia kutoka matumizi mengine na awe mpole asiropoke ropoke maana na yeye ataambulia ya vocha kidogo.
 
Kuna utetezi mreefu uliwahi kutolewa kuhusu picha ya tairi la ndege lililokuwa na mwonekano wa kuisha. Kwa mujibu wa yule bwana anasema ati tairi lina mzunguko wake hadi kuja kuisha na katika hali ile bado anasema lilikuwa halijamaliza mzunguko wake nikabaki nimeduwaa
Tairi bado wanalidai halijarudisha faida
 
Nimefanya kazi airport. Tena kitambulisho changu kilikuwa cha kufika karibu kila sehemu ndani kule ambako siyo wafanyakazi wote wa airports au wageni wanaruhusiwa kufika.
BTW, Mimi ni FOO/DISPATCHER.
Umewahi kufika airport?
 
WAHUSIKA WASOME UJUMBE HUU HARAKA!
NAFIKIRI UNGEULIZA TU; UTAJUAJE KAMA TAIRI LA NDEGE LINAHITAJI KUBADILISHWA
Jibu rahisi tu ni kuwa, ile tairi ni nene sana na uharibifu unaoangaliwa sana ni uliotokea pembeni (side ways)
Kama inaonekana kukatika/kukatwa huku pembeni au kama imeonesha kukatika sehemu ya kukanyagia kitu ambacho sio cha kawaida sana ndio hubadilishwa au basi isiwe na upepo wa kutosha kitu ambacho huonekana moja kwa moja kwenye dash board.
Vile vimstari vya kuzuia friction (kashata) ni vidogo sana kwa sababu kimsingi ndege inatakiwa ikimbie sana wakati wa kuondoka (take off) hivyo usiviangalie vile kutadhmini kuwa tairi imeisha
 
Usikute rubani alishatoa taarifa muda mrefu kuwa muda wa tairi kuruka na kutua umeisha, akajibiwa bajeti yake haijatengwa asubiri kidogo wataiandikia kutoka matumizi mengine na awe mpole asiropoke ropoke maana na yeye ataambulia ya vocha kidogo.
Rubani ndiyo anatoa taarifa za Technical issues za ndege au ni Mafundi waliosomea kazi hiyo?
 
Kuna utetezi mreefu uliwahi kutolewa kuhusu picha ya tairi la ndege lililokuwa na mwonekano wa kuisha. Kwa mujibu wa yule bwana anasema ati tairi lina mzunguko wake hadi kuja kuisha na katika hali ile bado anasema lilikuwa halijamaliza mzunguko wake nikabaki nimeduwaa
Swali la kujiuliza, tairi kama hilo lingetumika kwenye ndege inayombeba Rais wa nchi?

Kama jibu ni ndiyo, basi atakuwa sahihi. Lakini kama sivyo, lazima kuweko na mshangao!
 
Hutaki watoe maoni yao? Hata kama wamekosea. Hutaki kufahamu unaowapatia huduma wanauelewa gani kuhusu huduma yako?

Ofisi za umma, zinahudumia umma. Watumishi wengi wa umma ni wazembe na wavivu ndio maana hawataki wananchi watoe maoni kuhusu utendaji wenu.

Sikiliza, badilika. Sikiliza, elimisha. Mtumishi wa umma usikatae kusikiliza maoni ya wananchi.
📌🔨
 
Back
Top Bottom