kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Huku nyuma awamu ya 5 kila jaribio la wale nawaita wahuni kushika ndege za ATCL ili kulipwa madeni ya mchongo na Tanzania yamekua yanashindwa na ndege zimekua zinaachiwa baada ya muda mfupi. Wakati wa awamu ya 5 tuliona pale jaribio la kushika ndege ya ATCL kule afrika ya kusini liliposhindwa.
Wengi tunaamini hakuna mikataba na wawekezaji inafutwa kinyume na sheria za Tanzania ila wawekezaji hawaridhiki bila kuikomoa nchi kwa madai ya kutaka kuchuma utajiri bila ya kua wamewekeza kitu.
Pia wananchi wanaamini vigogo wenye nia ya kupiga hela ya umma hushirikiana na hao wanaodai ili kupewa fungu.
Tangu ndege ya ATCL ikamatwe uholanzi kwa kile kinasemekana ni serikali kudaiwa kimepita kipindi kirefu zaidi ya kama miezi sita. Kuna uvumi kwamba wapo vigogo wanakula njama na wageni hata kutaka kuuza ndege hiyo. Ingefaa kutolewa taarifa ya wazi nini kinaendelea kwenye hili sakata la kuzuiliwa ndege mali ya umma.