mlima wa mizeituni
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,387
- 2,444
Asante kwa ufafanuzi mzuri mkuu!Mkuu tuanze na huo mburuzo na ndio kuna issues nyingi. Miburuzo ya tairi ya ndege inasababishwa na tear and wear ya kawaida ya kuruka na kutua pia kuna mambo ya break za nguvu (harsh breaking) na hali ya njia ya kurukia ndege (runway surface condition). Mchubuko kwa mujibu wa document ya De Havilland ni ile hali ya kufikia nyuzi za tairi (reinforcement cord) siyo kipara cha kuisha michoro kama ilivyo kwa magari. Tuisome tena document ya De Havilland ili tujue wana maana gani unless english iwe imenipita pembeni. Mchubuko wa kwanza ukionekana anatakiwa asizidi miruko minane ndio maelekezo ya De Havilland. ukiangalia miruko ya ndege hiyo, miruko minane inaweza ikaisha kwa siku moja au mbili tu maana Dar kwenda Mwanza then Bukoba na kurudi ni miruko minne tayari na kama ataongeza kutoka Dar kwenda Mbeya na kurudi ni miruko miwil zaidi, na jumla itakuwa miruko sita kwa siku. Kwa kuangalia hiyo michubuko sio kuisha michoro ndege hiyo ina uwezo wa kutua tena mara saba bila matatizo. Nasema hivi kwa sababu kuna matabaka manne kabla ya kufikia sehemu ya upepo. Kwa maana hiyo, tairi ina usalama bado kutokana na muundo wake. ATCL, nikiangalia maelekezo ya De Havilland, huwa hawachongi (retreading) tairi zao zikiisha bali wanatupa. Kama wangekuwa wanachonga tairi zao wangepewa muongozo tofauti. Niseme tu tena kuwa huwezi ukahukumu kwa macho bila utalaam na uelewa wa maagizo ya watengenezaji. Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) hufuatia uelewa na utekelezaji wa hiyo miongo. Ukaguzi wa IATA (IATA Operational Safety Audit - IOSA) pia unajukumu la kuhakikisha ATCL wanakidhi matakwa haya na kinyume cha hapo wananyimwa cheti.
Nilianza mjadala kwa gadhabu lakini hukunipuuza wala kunichoka..
Umejibu kwa hekima sana na nimejifunza kitu kikubwa sana kutoka kwako!
Barikiwa!!