SoC02 Ndege ya Mizigo (Air Tanzania)

SoC02 Ndege ya Mizigo (Air Tanzania)

Stories of Change - 2022 Competition

Safari79

Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
6
Reaction score
7
Utangulzi

Kufuatia mpango wa serikali ya Tanzania kuagiza ndege moja ya mizigo (Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba tani 52) katika kkufanya biashara na kusaidia katika usafirishaji wa bidhaa za ndani na nje ya nchi. Niiliwaza na kuona kuwa kuna haja ya kulitizama hili mapema ili kuepuka hatua za zimamoto.

Maswali nnayo jiuliza mara wa mara
  • Je, hadi sasa muda wa ndege hii ya mizigo kuja Tanzania unajulikana ili utayari wa kazi uwe unajulikana?
  • Je, tumesha fahamu aina ya bidhaa ambazo ndege hii ya mizigo itakuwa inasafirisha kutoka ndani ama nje ya nchi?
  • Je, maongezi na watoa huduma haswa za ndani yameishaanza kufanyika ama kutiliana mikataba ya makubaliano kwa kuanzia?
  • Je, tumeweza vipi kujiapanga kibiashara ili pale ndege inapowasili nchini basi ikute maandalizi yote ya muhimu yamesha fanyika mapema?
  • Je, ni mizigo gani inayopelekwa nchi jirani ili kusafirishwa nje, nasi tuanze nayo kama bidhaa ya uhakika ya kusafiirishwa?
  • Taasisi za serikali kama za kodi, usalama, ukaguzi, wapakuaji wa mizigo wameongezewa nguvu na maarifa ili kuhimili ukuaji wa sekta?
  • Je, Wizara/Airtanzania imeshaanza kufanya upembuzi wa mahitaji na uwezo wa kusafirisha mizigo na kupata picha ya idadi ya miruko (routes)
Mawazo yangu Binafsi
  • Naamini vyama vya ushirika ama wakulima wakubwa wameanza kushirikishwa mapema ili pamoja na mambo mengine waweze kuwaunganisha wakulima kama wa matunda na mboga mboga haswa zaidi katika kutoa elimu ya kufungasha mizigo yao na katika kutafuta masoko ya nje mapema
  • Kwa kuwa MSD ilipewa jukumu la kusafirisha dawa katika nchi za SADEC, je maandalizi ya namna ya kusafirisha dawa yameanza kufanyika?
  • Kuna haja ya kuandaa vituo vya kuhifadhi mizigo ama majokofu yenye kuhifadhi baridi ili ubora wa bidhaa ubakie sawa sawa na mahitaji ya wasafirishaji?
  • Hali ya mikoa ikoje? Kuna bidhaa gani ukanda wa Mbeya zaidi ya maparachichi? Kilimanjaro maua? Dar es Salaam Samaki, Mwanza bidhaa za Samaki? Dodoma bidhaa za zabibu? Zanzibar viungo?
 
Upvote 1
Back
Top Bottom