Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Ndege moja ya mizigo ya Amazon Prime Air imepata ajali na kushika moto baada ya kupitiliza barabara ya kutulia (runway) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, Jumapili hii mchana (usiku wa Saa 3 Tanzania).
Ndege hiyo aina ya Boeing 767-300, iliyokuwa ikitokea San Juan (Puerto Rico) ni moja ya ndege za mizigo za Amazon ilikuwa ikiendeshwa na kampuni ya 21 Air, inasemekana ilipitiliza eneo la uwanja na kwenda kugonga magari barabarani ya nje ya uwanja huo majira ya saa nane mchana (saa 3 usiku huu kwa majira ya hapa kwetu).
Vitu muhimu juu ya ajali hii hadi sasa:
Msemaji wa Amazon, Kelly Nantel, amesema kuwa kwa sasa kipaumbele chao kikubwa ni usalama na afya ya wote waliohusika. Ameongeza kuwa wanafuatilia kwa karibu na mamlaka za eneo hilo ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo iliyotokea ghafla.
Licha ya kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa ndege za Boeing, lakini aina hii ya ndege haina historia ya kuhusishwa kwenye ajali za mara kwa mara. Boeing 767-300 ina kiwango cha juu cha usalama katika sekta ya usafiri wa anga (safety rating ya ajali ya chini 0.5 kwa kila safari milioni moja).
Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kubwa iliyoihusisha aina hii ya ndege ya mizigo ilikuwa ni ya Kampuni hii hii ya Amazon, mwaka 2019 (Atlas Air Flight 3591) iliyoanguka Texas na kusababisha vifo vya watu 3, Ambapo uchunguzi ulibaini chanzo kilikuwa makosa ya kibinadamu ya rubani na wala sio hitilafu ya kiufundi ya ndege hiyo.
NBC news
Yahoo News

- Uharibifu uliotokea: Video kutoka eneo la tukio zinaonyesha moshi mweusi ukitanda angani huku ndege hiyo ikiwa imeshika moto.
- Kusitishwa kwa Shughuli uwanjani hapo: Mamlaka za uwanja huo zimesimamisha safari zote za ndege kwa muda na kufunga njia zote za kurukia na kutulia.
- Majeruhi: Mamlaka ya Usafiri wa Anga (FAA) pamoja na uongozi wa uwanja wa ndege bado hawajathibitisha kama kuna majeruhi au vifo.