Biashara ya ndege ni kama biashara nyingine, ni ngumu.
Kutarajia faida ndani ya miaka miwili au hata mi5 ni kutojua biashara inavyoenda.
Biashara hii inahitaji long term planning, tunaingia kwenye biashara hii tukiwa tumezungukwa na washindani, hatawezi kupata faidi siku za karibuni. Ila kwa mipango na uendeshaji mzuri tutavuka.
Wengi hatujui faida ya ndege. Kwa ufupi kabisa, faida moja wapo ya ndege ni utalii na uwekezaji.
Ukipanda Kenya Airways, lazima itue Kenya, ukipanda Ethiopian Air lazima itue Ethiopia, sasa unatarajia vipi mtalii atue Kenya then apande nyingine kuja Tanzania kutalii? Kwa nini aangaike na asibaki kutalii Kenya?
Ndege zetu zitaleta watalii moja moja. Inaweza isiwe mwaka huu ila tutafika.
Uwanja wa ndege wa Nyerere umetanuliwa sana, je tunataka ujae na ndege za Kenya, Ethiopia, Rwanda na South Africa bila kuwa na Air Tanzania?
Yaani ni sawa kuwa nyumbani kwako kuna parking kubwa nzuri ila yana paki magari ya majirani tu.