Ndege ya Tanzania iliyokuwa imeshikiliwa Uholanzi yaachiliwa kwa kuilipa Eco Energy US$ 165M (403bn Tsh)

Ndege ya Tanzania iliyokuwa imeshikiliwa Uholanzi yaachiliwa kwa kuilipa Eco Energy US$ 165M (403bn Tsh)

Anachanganya watanzania wengi tunampenda kwa sababu ni social na good citizens kwenye mambo ya jamii (community issues) kama harusi, misiba, ku support local programmes ndogo ndogo ambazo viongozi wengine wa hadhi yake awatilii maanani.

Lakini aina maana kama kiongozi wa nchi alifanya kazi nzuri alikuwa raisi mmbovu mno; he will be doing us a lot of favour akijificha huko Msoga and no one will miss him.
Kuna vitu vingi jk naona Kama anazingiziwa tu mengine uongo sana
 
Kwanza ndege yenyewe haitengebezi faida, kila mara tunaambiwa wanaingiza hasara, si bora lichukuliwe tu kulikoni kuondoa 402B kwenye mzunguko w pesa nchini?

Unafikiri kulipa pesa nyingi kama hiyo haitaathiri mzunguko wa pesa nchini?
Uko sahih mkuu
 
Halafu leo eti uingereza inatoa msaada wa 15b kuipa tz, kumbe tunaouwezo wa kutoa 400b,aisee! Bongo inafurahisha mno.......
Tumekopeshwa na hao Ili kumlipa mhuni Ili ndege ilokamatwa kimagumashi irudishwe.
 
Msiwe wepesi kupinga uwekezaji wa bandarini. DPW akianza kazi mahali pale kwa mwaka mmoja TRA inakwenda kuingiza trilioni 26 kama kodi ya serikali.

Tutanunua ndege ngapi kwa pesa hizo?. Tutalipa madeni yote ya huko nje na chenji nyingi tu itabakia.
Ili tuwe wepesi kuukubali! Hayo mahesabu ya Trilioni umeyaona ndani ya mkataba!?Hata hujui mkataba utaisha lini!
 
Kuna Kila dalili mjadala kuhamia huko.

Tumalizane na HOJA ya Bandari kwanza, hizi zingine ziwe NYONGEZA.
 
Hiyo ndiyo Serikali ya CCM. $165 m inanunua ndege kama hiyo. Itajenga maelfu ya madarasa. 2025 siyo mbali tuungane CCM itoke madarakani.
 
Na viongozi wa upande ule pia waache ujuha wa kuliingiza taifa kwenye mikataba ya kimangungo
Kwenye hilo huna ushahidi, ni udini umekutangulia
Pole sana nchi ipo kwenye mikono salama, hakuna kutekana, hakuna kuchinjana, hakuna kuoneana, ni mikataba ya kimaendeleo tu kwa kwenda mbele, na nyie ikifika zamu yenu vunjeni mikataba kibabe kutafuta umaarufu na ikifika enzi yao watalipa faini na fidia maisha yanaenda
 
Kuna vitu vingi jk naona Kama anazingiziwa tu mengine uongo sana
Hana tofauti na Samia uongozi wao ni ‘laissez faire’; kuna mengi ya ovyo yanafanyika bila ya baraka zao.

Halafu ni easy to manipulate hasa kwenye uwekezaji usio na tija bila ya kuangalia picha kubwa na athari zake kwa jamii ata kama ni watu 100 watakao umia they don’t give a toss.

Yeye mwenyewe J.K anajua kwenye uongozi wake alizingukwa na watu waliokuwa wakimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa na bado akuwachukulia hatua ata alipobaini dhambi zao. Kwa hivyo lawama ni zake.

He was just a bad president.
 
tuanzie hapo, nani alisababisha kuvunja mkataba huo hadi tukala hasara hii. bilioni 400 na ushee tungejenga madarasa na hospitali ngapi? barabara ngapi ingejenga, afu mjinga mmoja tu anakuja kutusababishia hasara hiyo?
Waache walipe maana ata zikiwepo nchini wanagawana Wakubwa
 
Dawa ya deni kulipa.

Huwezi kukaribisha wawekezaji wakija kuwekeza halafu uwaambie "sitaki", lazima ile kwako kwa makubaliano ya Umoja wa Mataifa.

Moja ilishikwa Canada - tukalipa.
Nyingne ikashikwa Afrika Kusini - tukalipa.
Hiyo umeshikwa Uholanzi- tumelipa.


Tuliishika meli ya samaki, tukagawana samaki - tumelipa samaki, na meli na muda wote iliyokuwa imekaa kesi inaendelea.

Tuliowapora mali zao tukawalipisha "plea bargain" tumewalipa na bado tunaendelea kuwalipa.

WOTE HUO UJINGA WA MTU MMOJA, NA BADO MADUDU YATAENDELEA KUFUMUKA.
Bado dude la DPW,nyie jitoeni ufahamu.Hawa ndiyo watatutia umasikini totally!
 
Mkataba alioingia Kikwete akaja kuuvunja Magufuli, then huyo Kikwete "think tank" wa Samia tunaona mwanafunzi wake akitutoa sadaka kwa waarabu milele..

Naamini kabisa huo mkataba ulikuwa wa kinyonyaji kwa watanganyika kwa sababu Magufuli hakuwa na tabia za Kikwete na Samia, hao wawili ni waswahili selfish sana.
Nani aliyepitisha? Mawakili wa serikali walitoa ushauri gani? Nani anawajibika? Hatua zichukuliwe
Pia tujifunze kwani yaelekea tunaingia mkataba mwengine kama huu hapa bandarini
 
Hivi unafikiri ni nani analipa kama siyo na wewe?
Sina uhakika kama ubongo wako umetimia!! Haohao wananchi ambao wanapigia kelele kuhusu vifungu fikirishi juu ya DP world, still ww unakaza bichwa kuwapinga na kuwaona wana chuki!!!
 
Kuna Kila dalili mjadala kuhamia huko.

Tumalizane na HOJA ya Bandari kwanza, hizi zingine ziwe NYONGEZA.
Naunga Mkono hoja. Lakini, kwa maelezo yaliyopo ni kuwa hakuna kitakachobadilika maana wino umeisha mwagwa!!!

Kwa hiyo, hoja iwe ni namna gani matwakwa kutoka kwa baadhi ya wananchi yatatekelezwa bila kuathiri shughuli za kimaendeleo, na umoja wa kitaifa. Njia moja wapo baadhi wameanza nayo ni kwenda Mahakamani. Lakini, wakati huo, Chama kina himiza serikali itoe Elimu juu ya habari hii ya bandari.
 
Bado dude la DPW,nyie jitoeni ufahamu.Hawa ndiyo watatutia umasikini totally!
Wakutie umasikini mara ngapi? Hapo ulipo hohehahe.

Watu wanakuja kukufunguwa minyororo ya ujinga uliyonayo, wewe unaona wanakuja kukutia umasiki. Akili za kijinga hizo, kwa kuwa wewe mwizi unafikiri wote wezi.
 
By MMM

Watu wamepiga kelele kutaka kujua ndege imeachiwa kwa masharti yapi. Leo MMM ametutonya kama ilivyo hapo juu Walitaka walipwe US&500M (1.2 Trillion) wamelipwa 403 Bn Tsh.

Magufuli kwa ubabe alivunja mkataba na EcoEnergy ulioingiwa na Kikwete.
cae no. ICSID No. ARB/17/33

Serikali ya Samia imelipa.
Zingelijenga shule ngapi?
Dawa kiasi gani?
Mikopo ya wanafunzi kiasi gani?
Kama ni kweli si tungewaachia tu hiyo ndege kwa kuwa haifiki hiyo hela, maisha yaendelee baadae na sisi tuwadai ndege na hasara ya Mabilioni waliotusababishia kwa kushikilia ndege ikiwa kazini... labda kama kukamata mali ilikuwa sehemu ya mkataba
Ila pia ni fundisho la kuwa makini na mikataba ya kigeni kwa kuwa wenzetu wana janja janja nyingi
 
Back
Top Bottom