The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Muda kidogo uliopita, televisheni ya taifa ya Jordan iliripoti kwamba Jeshi la anga la Kifalme la Jordan limehusika katika operesheni na Umoja wa Falme za Kiarabu ya kudondosha "tani 25 za chakula cha msaada na vifaa muhimu vya kibinadamu" huko Gaza.
Ndege mbili za Jordan C-130 na ndege moja ya Umoja wa Falme za Kiarabu zilihusika katika operesheni hiyo na kulenga maeneo kadhaa ndani ya Ukanda wa Gaza, ripoti inasema.Picha zilizofikia chumba cha habari cha BBC kutoka kaskazini mwa Gaza, zinaonyesha watu huko Beit Lahia wakiwa wamebeba mifuko ya msaada.
Haya yanajiri kufuatia tangazo kutoka Israel la kusitisha mapigano katika baadhi ya maeneo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
Umati wa watu ulionekana wakipanda kwenye malori ya misaada na kubeba magunia makubwa mabegani mwao.