Ndege za Jordan na UAE zadondosha tani 25 za misaada huko Gaza

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Muda kidogo uliopita, televisheni ya taifa ya Jordan iliripoti kwamba Jeshi la anga la Kifalme la Jordan limehusika katika operesheni na Umoja wa Falme za Kiarabu ya kudondosha "tani 25 za chakula cha msaada na vifaa muhimu vya kibinadamu" huko Gaza.

Ndege mbili za Jordan C-130 na ndege moja ya Umoja wa Falme za Kiarabu zilihusika katika operesheni hiyo na kulenga maeneo kadhaa ndani ya Ukanda wa Gaza, ripoti inasema.Picha zilizofikia chumba cha habari cha BBC kutoka kaskazini mwa Gaza, zinaonyesha watu huko Beit Lahia wakiwa wamebeba mifuko ya msaada.

Haya yanajiri kufuatia tangazo kutoka Israel la kusitisha mapigano katika baadhi ya maeneo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.

Umati wa watu ulionekana wakipanda kwenye malori ya misaada na kubeba magunia makubwa mabegani mwao.
 
Hii ni kwa waarabu na mshirika wao kujivua lawama tu. na kuwapunguzia hasira watawala wa nchi hizo kutoka kwa wananchi wao wanaokasirishwa na jinsi falme hizo za kiarabu zinavyobehave.

Israel kawaruhusu wafanye hivyo ili kujisafisha maana kuna pressure kubwa kwa Israel hivi sasa kuhusu starvation inayoendelea huko Gaza. Hata vyombo vya habari vilivyokuwa vikifumbia macho ukatili wao kama vile BBC na CNN vimeanza kuwageuka.
 
Jitu jeusi Bana kwa ujuaji ujuaji Tu. Utakuta mwamba yuko zake Nyarugusu ndani ndani huko na Sijdah lake kuubwaa pajini kama chapati anailewa vema Jordan na UAE.
 
Tani 25 ha wanakijiji wa mpwayungu village hakiwatoshi kwa siku mbili
 
Israel imeruhusiwa kufanya inachotaka huko Gaza na hao hao wanaoipigia kelele Sasa iruhusu misaada kupita.
 
Na ni wanafiki sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…